Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 2, 2015

Watu wanne wafariki Dunia Baada ya Basi Kugonga Treni



Watu wanne wamefariki dunia  leo na wengine 21 kujeruhiwa  kufuatia basi aina ya Isuzu kugonga treni ya abiria  iliyokuwa ikienda bara katika kilomita 276/0 kati ya stesheni za Kimamba na Kilosa Mkoani Morogoro wilayani Kilosa majira ya saa 11:25 asubuhi ya leo.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elia Mshana imesema basi hilo lenye namba za usajili T 837 CTM Isuzu Coaster linamilikiwa na Feisal A. Khuwel wa Kilosa.
 
Taarifa kutoka eneo la tukio imefafanua kuwa waliofariki ni wanaume wawili, mwanamke mmoja na mtoto wa miaka minne. Kwa upande wa majeruhi, majeruhi 21 wako wanaume 14 na wanawake 7 ambao wanaendelea na matibabu katika Hospital ya Wilaya ya Kilosa.
 
Hata hivyo baada ya ajali treni ya abiria imeondoka katika stesheni ya Kilosa saa 3 asubuhi kuendelea na safari yake kwenda Bara.

0 comments:

Post a Comment

SHARE