
Msafara
 wa timu ya Taifa ya Tanzania (taifa Stars) inayodhaminiwa na kampuni ya
 bia ya Kilimanjaro Premium Lager tayari umewasili salama katika eneo la
 Borg El Arab jijini Alexandria na kufikia katika hoteli ya Panacea tayari kwa mchezo wake wa Leo.
Taifa
 Stars ambayo ilikuwa kambini nchini Ethiopia kwa takribani wiki moja, 
iliondoka juzi usiku Addis Ababa  na kuwasili uwanja wa ndege wa Cairo 
majira ya saa 8 usiku, kisha kuunganisha kwa usafiri wa basi mpaka Borg 
El Arab takribani masaa matatu.
Kocha
 mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij, atakiongoza kikosi chake katika mazoezi
 ya mwisho jana saa 1 usiku katika uwanja wa Borg El Arab kwa saa za 
Misri, sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Akiongelea
 mchezo wa kesho, Nooij amesema anashukuru kikosi kimefika salama nchini
 Misri na kipo katika hali nzuri, vijana wana ari na morali ya hali ya 
juu, anaamini leo timu itafanya vizuri katika mchezo huo dhidi ya 
wenyeji Misri.
Nooij
 amesema mchezo wa leo ni muhimu kwake, na kikosi chake kitacheza mpira 
wa kasi na pasi za haraka haraka, huku safu ya ushambuliaji ikihakikisha
 inatumia vizuri nafasi itakazozipata.
Aidha
 kuelekea katika mchezo huo wa Leo, kiungo Amri Kiemba ameungana na 
wachezaji wengine waliokuwa kambini Addis Ababa kuchukua nafasi ya 
Mrisho Ngasa ambaye alishindwa kuungana na timu kutokana na sababu 
zilizopo nje ya uwezo wake.
Naibu
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia tayari 
amewasili jijini Alexandria kwa ajili ya kuipa sapoti Taifa Stars katika
 mchezo huo wa leo.
Mchezo
 kati ya Misri na Tanzania utachezwa leo saa 2 usiku kwa saa za Afrika 
Mashariki na kati katika uwanja wa jeshi la Misri (Borg El Arab) uliopo 
takribani kilometa 70 kutoka jijini Alexandria na kilometa 200 kutoka 
jiji la Cairo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment