Pages

Ads 468x60px

Thursday, July 9, 2015

Prof. Mwandosya Awaangukiwa Wabunge wa UKAWA........Asema siyo Picha Nzuri Rais Kuvunja Bunge Bila Wabunge Hao



WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalum Prof.Mark Mwandosya amesema sio kitendo kizuri kwa wabunge wa upinzani kususia Bunge wakati Rais Jakaya Kikwete atakapokwenda kuvunja Bunge hilo leo.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma jana wakati akichangia Mswada wa Sheria wa Kuanzisha Tume ya Utumishi wa Walimu alisema si jambo zuri hata kidogo kwa jambo kubwa la Taifa kama hilo kufanyika bungeni lakini wabunge wa upinzani kutokuwepo.

Alisema tangu kuwepo kwa wapinzani katika Bunge hilo kumeimarisha demokrasia lakini kupingana kwa hoja ndio jambo la msingi lakini ni muhimu pia mawaziri wakahudhuria vikao vya Bunge.

Prof.Mwandosya alisema hili litakuwa Bunge lake la mwisho la kuwatumikia wananchi hasa wa Jimbo la Rungwe Mashariki kwa vipindi vitatu mfululizo na kuchaguliwa bila kupingwa 
 
"Ujio wa Rais ndani Bunge ni jambo zito na muhimu sana hasa kwa Taifa lakini haiwezekani Rais anakuja kuvunja Bunge wapinzani hawapo si jambo zuri lakini sio kila kitu kinacholetwa na Serikali lazima wapinzani wapinge wakati mwingine ni kushindana kwa hoja tu," alisema Prof.Mwandosya.

Alisema Demokrasia sio kupingana kila kitu lakini pia kwa Mswada huo wa kuanzisha Tume ya Walimu ni wazi kuwa Serikali inajali sana walimu kwani mishahara ya walimu italipwa na Serikali.

"Namshukuru sana Rais Kikwete na viongozi wengine kwa kunichagua mimi kuwa Waziri katika awamu tatu lakini pia nawashukuru wabunge wote kwa muda wote niliokaa hapa bungeni kwani sitakuwepo tena katika bunge lijalo na nimekuwa mbunge kwa miaka 15 sasa,"alisema Pfro.Mwandosya.

0 comments:

Post a Comment

SHARE