Nchi
za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania zinawasilisha bajeti zao kwa mwaka
wa fedha 2017/2018. Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango
anatarajiwa kuwasilisha bajeti hiyo bungeni leo mjini Dodoma kuanzia
saa 10 kamili jioni.
Kabla
ya kufanya hivyo, asubuhi Dk Mpango atawasilisha Taarifa ya Hali ya
Uchumi ya nchi, ambayo itajikita katika kueleza mipango ya maendeleo kwa
mwaka ujao.
Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge la Tanzania katika Mkutano wake wa Saba wa Bunge la Bajeti, wabunge watatumia kesho kusoma na kutafakari hotuba hiyo.
Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge la Tanzania katika Mkutano wake wa Saba wa Bunge la Bajeti, wabunge watatumia kesho kusoma na kutafakari hotuba hiyo.
Kuanzia
Jumatatu ijayo Juni 12 hadi Juni 20, mwaka huu, wabunge watajadili
Taarifa ya Hali ya Uchumi na Bajeti ya Serikali kwa siku saba kabla ya
jioni ya Juni 20, mjadala kuhitimishwa kwa upigaji kura ya wazi.
0 comments:
Post a Comment