TAARIFA KWA UMMA
Jeshi
la Kujenga Taifa (JKT), linapenda kuutaarifu umma kuwa limeongeza
majina ya vijana waliohitimu elimu ya kidato cha sita mwezi Mei 2017
kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.
Vijana hao wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia tarehe 13 Juni 2017 hadi tarehe 20 Juni 2017.
Mkuu
wa JKT, kwa mara nyingine tena, anawakaribisha vijana wote
waliochaguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza
uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa
kulijenga na kulitumikia Taifa letu.
Orodha
kamili ya majina ya vijana hao walioongezwa, maeneo ya makambi ya JKT
waliyopangiwa na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika
tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz . Usomapo tangazo hili mtaarifu na mwenzio.
BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA MAJINA YA VIJANA WALIOONGEZEWA NA MAKAMBI WALIYOPANGIWA
0 comments:
Post a Comment