Spika
wa Bunge, Job Ndugai amewakumbusha wabunge wa upinzani wanaotaka marais
wastaafu washtakiwe kuhusu sakata la mchanga wa madini, wakumbuke wanao
mawaziri wakuu wastaafu wawili ambao watahusika pia.
Ndugai
amesema hayo leo (Jumanne) bungeni baada ya mchango wa Mbunge wa
Kilombero, Peter Lijualikali kusema haiwezekani mawaziri na watendaji
wengine wa Serikali wakafanikisha mikataba mibovu ya madini bila ridhaa
ya Rais.
"Haiwezekani
mzee wangu (Andrew) Chenge na (Nazir) Karamagi walipitisha mikataba
hiyo bila Rais aliyekuwapo kufahamu. Kinga ya Rais kushtakiwa iondolewe
ili wahojiwe," amesema Lijualikali.
Baada
ya hoja hiyo ya Lijualikali inayofanana na ya Mbunge wa Tarime
Vijijini, John Heche, Ndugai aliwakumbusha juu ya mawaziri wastaafu
walionao kwenye chama chao.
"Mabadiliko mnayoyataka yakipitishwa na viongozi mlionao wakikamatwa msije mkalalamika tena," amesema Ndugai.
0 comments:
Post a Comment