Pages

Ads 468x60px

Tuesday, June 13, 2017

Jeshi la Polisi latoa tahadhali kwa wananchi, latoa onyo kali

Jeshi la Polisi nchini Tanzania limetoa tahadhari kwa wananchi kuwa ndani ya Jeshi la hilo hakuna ajira zilizotangazwa, na kuwataka wananchi wote kuwa makini na mtandao wa matapeli.

Tahadhari hiyo imetolewa na msemaji wa jeshi hilo, Advera John Bulimba – ACP kufuati kuibuka kwa kikundi kidogo cha matapeli wanaozunguka katika maeneo mbalimbali hususani vijijini na kuwalaghai vijana kwamba watawapatia ajira ndani ya Jeshi la Polisi jambo ambalo siyo la kweli.

ACP Bulimba amesema kuwa kikundi hicho cha matapeli kilichoibuka hivi karibuni kinazunguka maeneo mbali mbali na kuwadanganya vijana kuwa wao ni waajiriwa wa Jeshi la Polisi na kujipatia fedha kwa udanganyifu huo.

Amesema mfumo wa ajira ndani ya Jeshi la Polisi ni wa wazi na una utaratibu maalum ambao hutangazwa kwa wananchi kwa mujibu wa taratibu za Jeshi hilo.

Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa wote wenye tabia hiyo ya utapeli kuacha mara moja na endapo mtu yeyote atabainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Aidha, Jeshi hilo limetoa rai kwa wananchi wote wenye taarifa za matapeli hao kuzifikisha haraka katika kituo chochote cha Polisi kilicho karibu ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

0 comments:

Post a Comment

SHARE