Pages

Ads 468x60px

Friday, June 5, 2015

SAKATA LA UCHAGUZI 2015: Samwel Sitta achukua fomu, ataka miaka 5 tu kuwang’oa mafisadi



Waziri wa Uchukuzi Samweli Sitta akionesha fomu ya kugombea urais mara katika ukumbi wa NEC makao makauu Dodoma.
 
Waziri wa Uchukuzi Mh. Samweli Sitta akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu leo.

Waziri wa Uchukuzi  Mh. Samweli Sitta leo  amechukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya  chama cha Mapinduzi makao makuu ya CCM yaliyopo White House  Dodoma  mjini. Sitta ameambatana na Mke wake pamoja na wapambe wake.

Akizungumza mara baada ya kupokea fomu Sitta amesema kwamba  anaomba   miaka mitano tu sio zaidi ili aweze kuwashughulikia ipasavyo mafisadi na kumaliza kabisa tatizo la ufisadi  unao onekana kukwamisha maendeleo ya ya  nchi Hivisasa.

Aidha, ametaja vipaumbele vyake kuwa ni;

(i) Kuulinda muungano
(ii)  Kumalizia mchakato wa katiba Pendekezwa
(iii)  Kumaliza kabisa suala la Rushwa
(iv) Kuleta mahusiano mazuri kati ya  Wafanyabiashara na Serikali
(v) Kuimarisha Chama kiuchumi.

0 comments:

Post a Comment

SHARE