Swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, CHADEMA, Leticia Nyerere 
aliuliza endapo Serikali ina mpango wowote wa kuhalalisha matumizi ya 
bangi kitabibu. 
Mfano ulikuwa kutoka kwa Serikali ya Jimbo la DC nchini Marekani ambako 
hivi majuzi walipitisha matumizi ya bangi kama dawa na kilevi!
 
Majibu ya naibu Waziri wa Afya yaliweka msisitizo kwenye uharamu wa 
bangi kama isemavyo sheria ya Dawa za Kulevya ya mwaka 1971. 
Pamoja na kufafanua matumizi ya kitabibu ya Bangi bado msimamo wa Serikali ulikuwa ni kuiacha nbangi kuwa haramu. 
Ahsante Leticia kwa kujaribu!
SPIKA
 wa  Bunge, Anne Makinda amesema, bangi inayolimwa katika Mkoa wa Njombe
 si  kali kama inayolimwa mikoa mingine kutokana na baridi iliyopo 
mkoani  humo.
Makinda alijikuta akitoa jibu hilo huku akicheka kutokana na swali la  
nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Christowaja Mtinda  
(Chadema), ambaye alisema kuna baadhi ya maeneo nchini ukiwemo Mkoa wa  
Njombe na Mara, mmea wa bangi umekuwa ukiota bila kupandwa na hutumika  
kama chakula.
“Njombe bangi haioti yenyewe, tulikuwa tunapanda, lakini baada ya sheria
  iliyopitishwa mwaka 1975, tuliacha kupanda bangi, lakini hata hivyo  
bangi ya Njombe si kali kwa sababu ya baridi,” alisema Spika Makinda  
huku akiwaacha wabunge na wageni wengine wakicheka.
Katika swali hilo, Mtinda aliitaka Serikali kufanya utafiti ili mmea huo uweze kutumika kama dawa.
Hata hivyo, akijibu kwa Niaba ya Waziri wa Afya, Naibu Waziri wa Habari,
  Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia alisema Serikali haipo 
tayari  kuhalalisha matumizi ya bangi kama dawa kwa sababu athari zake 
ni  nyingi kuliko faida.
Awali, katika swali la msingi Mbunge  wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere 
(Chadema), alitaka kujua kuhusu msimamo  wa Serikali kuhalalisha matumzi
 ya bangi kama dawa kama ilivyofanya  Serikali ya Columbia iliyoruhusu 
matumizi ya bangi kwa ajili ya dawa.
Akijibu Nkamia alisema, msimamo wa  Serikali ni kwamba inafuata sheria 
inayoeleza kwa kina mtu yeyote  atakayejihusisha na kutumia, kuhamasisha
 matumizi, kuuza, kusafirisha,  kuhifadhi au kujihusisha kwa namna 
yoyote ile na bangi ni kosa la jinai.
“Adhabu ya makosa hayo ni kufikia hadi kifungo cha maisha. Napenda  
kushauri na kusisitiza bangi ni miongoni mwa dawa za kulevya ambazo  
tusizizalishe wala kuzisambaza kwa sababu madhara yake ni makubwa kwa  
afya ya binadamu,” alisema Nkamia.
Source : JamboLeo
 
0 comments:
Post a Comment