Mkazi wa Ilembo wilayani Mpanda , Petro Magawe (40) amejinyonga kwa kujitundika mtini akitumia shati lake.
Mtu huyo alijinyonga hadi kufa saa 2 asubuhi juzi karibu na Ofisi ya Misitu iliyopo Mtaa wa Majengo A mjini Mpanda.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari alisema Mei 30
, mwaka huu, Magawe alifika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Mpanda
mjini Mpanda, akieleza kuwa alikuwa akihitaji kuwekwa mahabusu .
“Badala ya kukubali ombi lake la kuwekwa mahabusu alipata msaada kwa
kupewa Fomu ya Polisi namba 3 ( PF 3) ili akatibiwe hospitalini baada ya
kuonekana kuwa alikuwa amechanganyikiwa kiakili,” alisema Kamanda.
Alisema “Siku iliyofuata asubuhi mtu huyo alikutwa amejinyonga kwa
kutumia shati lake mwenyewe.” Alisema polisi inaendelea na uchunguzi wa
tukio hilo .
0 comments:
Post a Comment