Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 3, 2015

Mgombea Urais UKAWA Kujulikana Mwezi Huu HEBU CLICK HAPA>>>>



MWENYEKITI wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amesema mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) atapatikana wakati wowote kuanzia sasa ndani ya mwezi huu.

Mbatia alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam juzi wakati akihojiwa katika Kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV.
 
Alisema mchakato wa kumpata rais ndani ya umoja huo unakwenda vizuri na hilo linatokana na UKAWA kuaminiana.

Alisema kuwa wapo watu wengi ndani ya UKAWA wanaoweza kugombea nafasi ya urais na si lazima rais awe mwenyekiti wa chama chochote. "Naomba tofauti zisiwepo ndani ya UKAWA ili tuweze kumpata mgombea mmoja wa nafasi ya urais ambaye atakuwa mwadilifu na mzalendo kwa taifa lake," alisema Mbatia.

Alisema yeye binafsi yupo tayari kutogombea nafasi yoyote hata ya udiwani iwapo hatapewa nafasi ya kuratibu shughuli za uchaguzi ndani ya umoja huo ili kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri.

Alisema hali halisi inaonyesha kwamba Watanzania wengi wanapenda UKAWA kuliko chama kimoja, hivyo ni lazima viongozi wa umoja huo kutambua kwamba wasiingize tofauti zao.

Alisema kwa asilimia 90 UKAWA imekamilisha taratibu za kuwapata wagombea katika baadhi ya majimbo na kata kwa ngazi za ubunge na udiwani, hivyo aliwataka Watanzania kuwaunga mkono kwa jitihada zao.

Alisema kuwa UKAWA si mali ya chama, bali ni mali ya Watanzania wote na kuwataka  wanachama wa CCM wenye nia njema kujiunga na umoja huo sasa na kutosubiri hadi washindwe ndani ya CCM.

Kuhusu vikundi vya ulinzi ndani ya vyama, Mbatia alisema kuwa vikundi hivyo havikuanzishwa kwa nia mbaya lakini viongozi waliopo madarakani wanavitumia kwa nia mbaya na kuwataka viongozi hao waliopo madarakani kuonesha mfano.

Alisema viongozi waliopo madarakani wanavitumia vikundi hivyo pamoja na Jeshi la Polisi kulipiziana kisasi na kuwataka  waliopo madarakani kuwa waadilifu. 
 
Kuhusu bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2015-2016, alisema bajeti hiyo ni ya maumivu kwa Watanzania wa hali ya chini kwa kuwa bajeti hiyo imejikita zaidi kwenye matumizi ya Serikali.

"Hizi bajeti zinazoendelea kujadiliwa bungeni ni bajeti za matanuzi kwa viongozi wa serikali lakini kwa Watanzania wa hali ya chini ni ya maumivu, Watanzania wategemee hali mbaya kwenye huduma za jamii," alisema.

Alisema rushwa ni tatizo kubwa ambalo linachangia mapato ya Serikali kutoonekana ambayo inasababisha watu matajiri kutolipa kodi na badala yake wafanyabiashara ndio wanakamuliwa.

0 comments:

Post a Comment

SHARE