Zoezi la Uandikishaji daftari la kudumu la wapiga Kura linatarajia kuanza katika mikoa ya Geita, Simiyu, Mwanza na Shinyanga, zoezi litakaanza rasmi tarehe 2/06/2015 hadi 04/07/2015.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya uchaguzi
imebainisha kuwa zoezi hilo litafanyika kwa kutumia teknolojia ya BVR
(Biometric Voters Registration.Vituo vya uandikishaji vitakuwa kwenye
vitongoji, mitaa na Vijiji katika kata zote za mikoa hiyo iliyotajwa
hapo juu na vituo vifunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa
12:00 jioni.
Watakaohusika ni;
Waliotimiza miaka 18 na watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi oktoba 2015.
Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la kudumu la wapiga ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya.
Wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika kwenye vituo vilivyoko ndani ya kata zao.
0 comments:
Post a Comment