Pages

Ads 468x60px

Wednesday, May 27, 2015

Tuhuma Za Sitti Mtemvu Kudanganya Umri, Kuitwa "Bibi Bomba" na Kutembea Na Baba Yake Zamuathiri Kisaikolojia Mdogo Wake



Aliyekuwa mshindi wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amekiri kuumizwa na kashfa mbalimbali zilizoandikwa kwenye vyombo vya habari ambazo zilipelekea familia yake kutawaliwa na huzuni jambo ambalo lilisababisha kuvua taji hilo.
 
Amesema tuhuma hizo zilimuumiza sana hasa baada ya mdogo wake wa mwisho kutaniwa na wanafunzi wenzake wakidai kuwa amekuwa akiwadanganya Sitti, ni dada yake kumbe ni mama yake mzazi.
 
Amesema kuwa ilifika wakati akiwa anaenda kumchukua mdogo wake shuleni marafiki wa mdogo wake walikuwa wanamtania wakidai mdogo wake ni mtoto wa ‘bibi bomba’ wakimaanisha yeye jambo ambalo mdogo wake lilikuwa linamuumiza sana.
 
Ameongeza kuwa kuna kipindi mdogo wake alikataa kwenda shule kutokana na utani kuzidi pia magazeti kuandika kuwa Sitti, ana uhusiano na baba yake mzazi jambo ambalo lilimuathiri sana mtoto huyo.

0 comments:

Post a Comment

SHARE