Hakika Mungu ni mwema sana. Ametuwezesha leo kuwa na nguvu ya kutafakari hatima ya nchi yetu ambayo inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 hapo Oktoba.
Mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia makada 
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakijitokeza kuwania urais kupitia chama 
hicho na tayari wameanza kuchuana kutangaza nia yao baada ya vikao vya 
Kamati Kuu Taifa (CC) na Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kumalizika hivi 
karibuni mjini Dodoma na kutoa baraka zote kuanza rasmi kwa mchakato 
huo.
Ninachowaomba watangaza nia ni kwamba wasitumie mwanya huo wa 
kujitangaza kuchafua wenzao na badala yake wajenge hoja bila kupitiliza 
kwa sababu kampeni rasmi zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi 
bado hazijaanza.
Kila mtangaza nia anatakiwa ajipange  kuwaeleza
 Watanzania jinsi ya kuboresha maisha duni ya wananchi kwani walio wengi
 ni magumu.
Watangaza nia wajipange kueleza jinsi ya kuondoa mfumuko wa bei za 
bidhaa mbalimbali nchini ambao uko  juu, wajipange kueleza wataisaidiaje
 jamii? 
  
Niwaase watangaza nia hasa kutoka chama tawala CCM kwamba kila neno watakalokuwa wanalitamka litakuwa linapimwa na wananchi.
Niwaase watangaza nia hasa kutoka chama tawala CCM kwamba kila neno watakalokuwa wanalitamka litakuwa linapimwa na wananchi.
Kwa hiyo basi, watangaza nia watakaotumia majukwaa kuwachafua wenzao,
 moja kwa moja watakuwa wamekwenda ‘nje ya reli’ kwa sababu sasa hivi 
wananchi wanataka kiongozi ambaye ataeleza jinsi ya kuwakwamuwa 
kiuchumi, kimatibabu na kielimu.
Ni jambo la msingi sasa kwa wana CCM kupima wagombea wao na 
wasijazane tu kwenye mikutano ya kutangaza nia na kushangilia kishabiki 
bila kupima neno kwa neno. 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment