Wanaotangaza Nia ya Urais Wasichafuane na Kupakana Matope na Badala yake Wajipange Kuwaeleza Watanzania Jinsi ya Kuboresha Maisha Yao
Mpekuzi blog
Hakika Mungu ni mwema sana. Ametuwezesha leo kuwa na nguvu ya kutafakari hatima ya nchi yetu ambayo inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 hapo Oktoba.
Mwishoni mwa wiki iliyopita tulishuhudia makada
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakijitokeza kuwania urais kupitia chama
hicho na tayari wameanza kuchuana kutangaza nia yao baada ya vikao vya
Kamati Kuu Taifa (CC) na Halmashauri Kuu Taifa (NEC) kumalizika hivi
karibuni mjini Dodoma na kutoa baraka zote kuanza rasmi kwa mchakato
huo.
Ninachowaomba watangaza nia ni kwamba wasitumie mwanya huo wa
kujitangaza kuchafua wenzao na badala yake wajenge hoja bila kupitiliza
kwa sababu kampeni rasmi zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi
bado hazijaanza.
Kila mtangaza nia anatakiwa ajipange kuwaeleza
Watanzania jinsi ya kuboresha maisha duni ya wananchi kwani walio wengi
ni magumu.
Watangaza nia wajipange kueleza jinsi ya kuondoa mfumuko wa bei za
bidhaa mbalimbali nchini ambao uko juu, wajipange kueleza wataisaidiaje
jamii?
Niwaase watangaza nia hasa kutoka chama tawala CCM kwamba kila neno watakalokuwa wanalitamka litakuwa linapimwa na wananchi.
Niwaase watangaza nia hasa kutoka chama tawala CCM kwamba kila neno watakalokuwa wanalitamka litakuwa linapimwa na wananchi.
Kwa hiyo basi, watangaza nia watakaotumia majukwaa kuwachafua wenzao,
moja kwa moja watakuwa wamekwenda ‘nje ya reli’ kwa sababu sasa hivi
wananchi wanataka kiongozi ambaye ataeleza jinsi ya kuwakwamuwa
kiuchumi, kimatibabu na kielimu.
Ni jambo la msingi sasa kwa wana CCM kupima wagombea wao na
wasijazane tu kwenye mikutano ya kutangaza nia na kushangilia kishabiki
bila kupima neno kwa neno.
0 comments:
Post a Comment