Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira leo
amekabidhiwa fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
huku kipaumbele chake kikubwa kikiwa ni kuinua kilimo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari hivi sasa katika ukumbi wa
mikutano wa makao makuu Wassira amesema ikiwa atachaguliwa kuwa rais
ataboresha kilimo kwa kutumia zana za kisasa huku akisisitiza kuwa
jembe la mkono litawekwa katika vyumba ya makumbusho ili iwe historia.
Kwa upande wa ufisdi amesema ufisadi ni wizi,anausikia tu na kwa
sababu atakuwa rais atahakikisha kuwa anawachukulia sheria pamoja na
kuziongea nguvu sheria ili kupambana nao.
Akizungumzia Muungano amesema atatetea na kuulinda maana kuuvunja ni kugawa nchi.
0 comments:
Post a Comment