MAMA
wa mtoto aliyeibwa kabla hajatimiza mwezi tangu azaliwe, Fatuma Bakari
ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Ilala jinsi mtoto huyo alivyoibwa na
mshtakiwa Neema Patrick.
Shahidi
huyo na mwingine walitoa ushahidi wao jana mbele ya Hakimu Adelf
Shachore kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Anunciata Leopold.
Awali
mashahidi hao walikuwa watano ambao walifika mahakani kwa ajili ya
kutoa ushahidi, lakini Wakili Leopold, alidai kuwa kwa mujibu wa shtaka
hilo waliotakiwa kutoa ushahidi walikuwa wawili tu.
Wakitoa
ushahidi wao mashahidi hao ambao ni Fatuma Bakari na Zainabu Said, wote
walikiri juu ya mtuhumiwa kufanya kitendo hicho cha kuiba mtoto.
“Ni
kweli siku ya tukio ambayo ni mwezi machi mwaka huu, mtuhumiwa
alinisindikiza hospital nilipokuwa naumwa jino, kutokana na hali
niliyokuwa nayo mtuhumiwa aliniomba anibebee mwanangu (Ibrahm Abdalah,
ambaye hajatimiza hata mwezi) lakini mara baada ya kufika hospital
maeneo ya Mbagala, Dar es Salaam, alishushuka haraka na kukimbia na
mwanangu,” alidai Shahidi huyo.
Awali
mashahidi hao walitakiwa kuwa watano lakini wakili wa serikali
alipinga kutoa utetezi wao, hivyo mashahidi watatu walibaki ushahidi wao
utasikilizwa Juni 24 mwaka huu.
Mtuhumiwa
huyo anadaiwa kumwiba mtoto huyo maeneo ya Mbagala Machi 3 mwaka huu
ambapo alikuja kukamatwa baad ya wiki mbili maeneo ya Ukonga Banana
akiwa na mtoto huyo, mtuhumiwa huyo yuko nje kwa dhamana.
0 comments:
Post a Comment