Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari Ambapo amesema
atachukua sehemu ya mshahara wake kwa ajili ya kuwalipa wanasheria
watano watakao kuwa wanafanya kazi ya kusikiliza na kuwasaidia wananchi
wenye migogoro ya ardhi.alitoa kauli
hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya
utatuzi wa migogoro ya ardhi katika wilaya yake ya Kinondoni Dar es
Salaam ."Kama nilivyobadilisha mfumo
mzima wa PF3 ndivyo ninavyofanya kwenye ardhi nimechukua hatua mahususi
kuchukua sehemu ya mshahara wangu na kuajiri jumla ya wanasheria watano
watakao wasaidia wananchi hasa wanyonge kupata haki zao juu ya madai yao
mbalimbali yahusuyo ardhi"
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda Akieleza zaidi Amesema wanasheria
hao watachukua asilimia 75 ya mshahara wake kwa kazi hiyo hivyo
mwananchi wa Wilaya ya Kinondoni hatatakiwa kulipa hata senti tano
atakapokuwa amekwenda kupata huduma hiyo.
Makonda
alisema kuwa kuanzia Jumatatu ya Juni 15, 2015 wanasheria hao watakuwepo
ofini kwake watakaofanya kazi saa zote kwa lengo la kusaidia ili wapate
uelewa wa kisheria juu ya haki zao zozote kuhusu umiliki wa ardhi.
Makonda
alisema heshima aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete ya kumteua kuwa mkuu wa
wilaya hiyo kwake anatafsiri kama changamoto kubwa ya kuhakikisha
anashughulikia kwa kina matatizo ya msingi ya wilaya hiyo
Alisema
katika wakati huu huwezi kutaja changamoto kubwa tatu za wilaya hiyo
ukaacha kutaja migogoro ya ardhi na kuwa kwa ufafanuzi zaidi unaweza
kurejea hotuba yake ya Februari 28, 2015 wakati akianza kazi mambo
aliyoyataja na kuyapa kipaumbele ambapo alitenga kila siku ya Ijumaa
kuwa ni siku ya kukutana na watu wenye migogoro ya ardhi ili kuitatua.
Makonda
alisema ili kumaliza changamoto hiyo ya migogoro ya ardhi kama si
kuipunguza kwa kiwango cha juu kila mkazi wa wilaya hiyo anatakiwa
kuchukua kopi ya hati au nyaraka yoyote ile inayompa uhalali wa kumiliki
ardhi, shamba au kiwanja na kopi hizo zipelekwe kwa ofisi ya mtendaji
wa kata kwani kuanzia Julai 2, 2015 yeye na timu ya watu wa ardhi
atahamishia ofisi yake kwenye kata hizo kwa ajili ya kuzihakiki nyaraka
hizo.
Alisema
pindi watakapo baini kuwa kiwanja kimoja kina zaidi ya mmiliki mmoja
watamtafuta mmiliki halali kupitia vyombo walivyonavyo na atakayebainika
ameghusi atachuliwa hatua.
Alisema
lengo la kuhamishia ofisi yake kwenye kata ni kufuta kabisa uzoefu wa
kusikitisha wa wananchi mmoja kugundua kwamba kiwanja chake kinamilikiwa
na mtu mwingine baada ya kumwaga roli la mchanga ama tofali.
Wanahabari wakiwa katika mkutano na Bwana Makonda.
Waandishi wa habari kutoka vyombombalimbali wakichukua taarifa hiyo
0 comments:
Post a Comment