WAENDASHA
pikipiki 100 wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wametakiwa kuacha
kuchukulia mambo ya siasa katika mafunzo wanayopewa na wataalamu wa
usalama barabarani kwa vile elimu wanayoipata iatawasaidia katika
kujikinga na ajali zisizokuwa za lazima.
Hayo
yalisemwa jana na Diwani wa Kata ya Kahama Mjini, Abas Omary
alipofunga mafunzo ya siku mbili ya bodaboda yaliyotolewa na wataalamu
kutoka Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Dare es Salaam.
Alisema
mafunzo hayo ni kwa manufaa ya waendesha pikipiki na si wanasiasa
hivyo ni bora wanaposikia kuna mafunzo kujitokeza kwa wingi hali
ambayo itachangia kupata elimu sahihi ya kuhusu usalama barabarani.
“Ninawaomba
bodaboda mnaposikia kuna mafunzo ya usalama barabarani ni bora
mkajitokeza kwa wingi kwa sababu katika mafunzo haya lengo ni kutoa
elimu kwa watu zaidi ya 200 lakini kwa sasa ni madereva 100 ndiyo
walijitokeza,”alisema.
Mkufunzi
kutoka NIT, Charles Kisunga, ni bora mafanikio yakaonekana
ikizingatiwa watu hao wamekuwa ndiyo chanzo kikuu cha ajali barabarani.
Alisema
mafunzo hayo ni maombi kutokaSerikalini na hadi sasa yametolewa
Mtwara kwa washiriki 600, Lindi na Sengerema mkoani Mwanza.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Kahama, James Lembeli, ambaye ndiye mfadhili mkuu wa
mafunzo hayo, alisema lengo kuu ni kuhakikisha bodaboda wanaepukana na
ajali kwa kufuata sheria za usalama barabaarani kwa usahihi.
0 comments:
Post a Comment