Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewataka watanzania
kuipinga na kutoikubali sheria ya mpya iliyopitishwa ya takwimu kwa
madai kwamba sheria hiyo inalenga kuzuia uhuru wa vyombo vya habari na
kuwanyima watanzania haki na uhuru wa kupata habari.
Akihutubia hivi karibuni mjini Bukoba katibu mkuu wa chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema Dk. Wilibroad Slaa alisema kupitishwa
kwa sheria hiyo kunalenga kunyima uhuru wa habari pamoja na kuwafanya
watanzania kuendelea kubaki gizani na kuishi kama wapo shimoni bila
kuelewa maovu yanayofanywa na viongozi wasio waadilifu wanaotumia
madaraka vibaya kwa masalahi yao binafsi.
Alisisitiza kuwa nia ya serikali kutaka kuzuia uhuru wa vyombo vya
habari ni kuwarudisha nyuma watanzania ili waweze kuishi bila kupata
habari kama ilivyokuwa enzi za ukoloni na kwamba hali hiyo haiwezi
kuvumiliwa kwani serikali inataka kuficha maovu ambayo yanaweza
kuliangamiza taifa hapo baadae.
0 comments:
Post a Comment