UKISTAAJABU
ya Musa utayaona ya Farao! Kumekuwa na madai ya baadhi ya wanafunzi wa
shule za msingi mjini hapa kujiuza kwa waendesha bodaboda kwa gharama ya
shilingi elfu mbili tu. Mwanafunzi
anayedaiwa kujiuza kwa waendesha Bodaboda.
Kufuatia madai hayo,
mwandishi wa kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ mjini hapa
alifanyia kazi madai hayo na kufanikiwa kumnasa Ally Shabani (34) ambaye
ni dereva wa bodaboda akiwa na mwanafunzi wa darasa la nne, Shule ya
Msingi ya Kiwanja cha Ndege mkoani hapa (jina tunalo).Tukio hilo la
kushangaza na kusikitisha pia, lilijiri Jumamosi iliyopita saa 7 mchana
katikati ya mashamba ya mkonge yaliyopo Kihonda Kwachambo ambayo
yanamilikiwa na Jeshi la Magereza jirani kabisa la Gereza la Kihonda
MAMA MZAZI AISAKA OFM
Awali,
mama mzazi wa denti huyo, Mariam Jongo alimtafuta Kamanda wa OFM Mkoa
wa Morogoro na kumweleza kuhusu tabia ya bodaboda huyo na mwanaye,
alisema:
”Naomba msaada wako baba, kuna dereva wa bodaboda nimempa tenda ya kumpeleka mwanangu shule.
“Lakini
cha ajabu nasikia anamshawishi mwanangu mwenye umri wa miaka 9 ambaye
hata maziwa hayajaanza kutoka kifuani ili afanye naye mapenzi akitumia
chambo cha shilingi elfu mbili, hivyo naomba msaada wako kama kamanda wa
kufichua maovu.”
Waliponaswa kichakani. OFM YATOA MBINU
Kamanda
wa OFM alimpa maelekezo mama huyo ya kutafuta vijana wa polisi jamii wa
kata ambapo baada ya kupatikana mwandishi wetu alimpa maelekezo denti
huyo na baadaye kwa kushirikiana na polisi jamii na OFM walitega mtego.
DENTI AMPIGIA BODABODA
OFM
alimuita denti huyo na kumpa simu ili ampigie bodaboda huyo ambapo
alimtaka aende kijiweni kwake Kihonda kwa Chombo, Mwisho wa Hiace. Denti
alilazimishwa na mama yake afike kwenye kijiwe hicho akiwa anafuatwa
kwa karibu na OFM na polisi jamii.
BODABODA AMPANDISHA DENTI KWENYE BODABODA
Bila
kujua kuwa yupo kwenye mtego, bodaboda huyo alimpakia denti ambaye
alionywa kutosema kuhusu mtego na kuondoka naye huku akiendelea
kufuatiliwa kwa nyuma na kikosi kazi hicho.
Alipofika jirani na
Barabara ya Mazimbo, alisimama, akataka kuingia naye gesti lakini
akajishtukia kwa vile ilikuwa mchana na jua kali.
Dereva bodaboda Ally Shabani aliyedaiwa kukutwa na mwanafunzi akiwa mikononi mwa wananchi.
AAMUA KWENDA MKONGENI
Bodaboda
huyo alipoona ilikuwa vigumu ‘kujitoma’ gesti na mtoto wa watu,
alielekea kwenye shamba la mkonge lililoko kando ya Barabara ya Dodoma
na kuzama ndani.
Njemba huyo alijiongeza kwa kusimamisha bodaboda
katikati ya shamba na kukaa chini na mtoto huyo ambapo walianza ‘love
story’ kwanza.
OFM HIYO!
Ndani ya dakika 10 tu, OFM na kundi lake
waliwavamia kwa nyuma na kumkamata bodaboda huyo na kumuuliza kisa cha
kuangukia kwa mtoto kama huyo ambaye ni sawa na mwanaye wa kumzaa akiwa
ameshamkatia shilingi elfu mbiliUTETEZI WAKE
Katika utetezi wake,
bodaboda huyo huku akiangua kilio alimtupia lawama shetani na kuomba
msamaha akisema yeye ni mume wa mtu na mkewe analea!
”Shetani
kanipitia jamani, mke wangu analea mtoto wetu wa mwisho ana mwaka mmoja
kasoro, naombeni msamaha yaishe hapahapa, mnifichie aibu hii,” alisema
bodaboda huyo.
WATU KIBAO
Baada ya muda habari za bodaboda huyo
kufumwa zilisambaa kwa kasi ya upepo na watu kibao walifurika kwenye
shamba hilo huku baadhi ya bodaboda wenzake kwa hasira walimshushia
kichapo mwenzao huku baadhi wakitaka kumuua.
Binti huyo akiwasili kijiweni. POLISI WAITWA
Baada ya kuona jamaa anaweza kuuawa, OFM waliita polisi wa pikipiki ambapo kwa mshangao, mmoja wa polisi hao alisema:
”Sisi tuna bifu na bodaboda baada ya mwenzetu kupigwa kule Mindu. Kama unaweza mpakie kwenye pikipiki yako mlete kituoni.”
Ilibidi
OFM iite askari magereza ambao walimchukua bodaboda, denti na mzazi
wake na kwenda ofisi zao zilipo jirani na shamba hilo.
Baadhi ya watu, hasa wanawake waliokuwepo eneo hilo walisikika wakisema huenda bodaboda huyo alikuwa na lengo la kishirikina.
”Hii
siyo bure hiki kitoto kinajua nini katika mapenzi. Huyu huenda ametumwa
na mganga wa kienyeji. Sisi wamama tuko hatuna waume ameshindwa nini
kuja... kwetu?” alihoji mwanamke mmoja.
...Wakiondoka. MADAI YA KUJIUZA
Kwa
mjini Morogoro, baadhi ya bodaboda wanadaiwa kutumia nafasi ya kuwa na
chombo hicho cha usafiri kuwalaghai wanafunzi wa shule za msingi kwamba,
wakilala nao watakuwa wanawapakiza kwenda shule na pia kutumia shiling
elfu mbili kama chambo kikubwa.
“Kwa sasa mjini Morogoro madenti wa shule za msingi kujiuza ndiyo fasheni, wanarubuniwa na shiling elf
Monday, May 25, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment