Ni vigumu kuamini! Bwana harusi Abasi Khamis Abdallah amejikuta akizimia
zaidi ya mara tatu baada ya kubaini kuwa, bi harusi, Fatuma Salum Omar
aliyefunga naye ndoa ni mke wa mtu na ana watoto wanne, Amani lina mkasa
kamili.
Ilielezwa kwamba, Abasi alimuomba Fatuma wafunge ndoa lakini mwanamke huyo aliomba apewe miaka miwili akidai kwa wakati huo anasoma kidato cha pili.Miaka miwili ilikatika huku wawili hao wakiwa kwenye mapenzi, Abasi akijua kuwa ‘mtu’ wake anamalizia masomo.Hata hivyo, ilipofika siku ya matokeo ya kidato cha nne, Abasi aliomba kujua matokeo na kuhoji mbona haoni jina lake (Fatuma)!!
Ilidaiwa kuwa, Fatuma alimzuga kuwa alikatiza masomo dakika za mwisho hivyo dada yake akampeleka chuo.
Siku ya kupeleka posa ilipofika, Abasi alimuomba Fatuma ampeleke kwa wazazi wake, akamwambia awasiliane na dada yake, kumbe Fatuma alimpa dada feki ambaye aliongea na Abasi na kumwambia ampe siku mbili.
“Zilipita siku kama nne, tukamtafuta tena Fatuma na kumwambia aseme kama hataki ndoa kwani siku zinaenda na watu wameshajipanga na dada hajasema chochote, akajibu atatupeleka kwa shangazi yake ambaye anakaa Kigamboni (Dar).
“Cha kushangaza siku ya ndoa haijafika, tukapigiwa simu
wakiomba ile fedha iliyobaki (laki mbili) itumwe kwa huduma ya mtandao
wa simu, wakasumbua sana kisha tukaituma,” alisema mama wa Abasi
aliyejitambulisha kwa jina moja la Fauzia .Siku ya ndoa ilipofika, Abasi
na ndugu zake walikwenda kuoa, cha kushangaza walipokuwa
njiani waliambiwa waende msikitini ingawa kuna watu waliokuwa wameshatangulia nyumbani, wakadai kuwa hakukuwa na dalili ya mtu kuonesha kuwa kuna sherehe.Walipofika msikitini, Mburahati walifunga ndoa ingawa shehe alitia shaka na kumuuliza Fatuma kama ni mjane kwani wapo watu waliomtonya kuwa ni mjane.
Fatuma alikana si mjane, ndoa ikafungwa kwa shaka huku shehe akiendelea kujiridhisha.
Fauzia alisema kuwa baada ya ndoa, watu walitimba Kigamboni kwa ajili ya sherehe ndipo baadhi ya waalikwa waliporopoka kwamba, Fatuma ana watoto wanne na ni mtalaka aliyeachwa siku sita zilizopita hivyo bado yupo eda.
Kikao cha familia kilipokaa, mume wa Fatuma (baadaye iligundulika jina lake ni Asha) wa kwanza aliyejulikana kwa jina moja la Masoud alifika na kukiri kuwa alimuoa Fatuma na amezaa naye watoto wanne.
Tukio
hilo la kihistoria lilijiri hivi karibuni, Kigamboni, Dar mara tu baada
ya ndoa hiyo kufungwa msikitini ambapo wazazi wa bwana harusi ndiyo
waliotonywa kuhusu siri hiyo.
Bwana harusi Abasi Khamis Abdallah na
bibi harusi wakiwa na nyuso za furaha siku ya ndoa yao. Awali, kabla ya
ndoa, wazazi wa bwana harusi walimchunguza Fatuma, akawaambia yeye bado
ana ‘usichana’ wake hali iliyowaridhisha kuwa wamepata mkwe bora.
Simulizi hiyo ya aina yake ilieleza kwamba, Fatuma na Abasi walikutana
kwa mara ya kwanza mwaka 2013 bandarini jijini Dar ambapo mwanamke huyo
alikuwa akitoa mizigo, wakazama kwenye mapenzi.Ilielezwa kwamba, Abasi alimuomba Fatuma wafunge ndoa lakini mwanamke huyo aliomba apewe miaka miwili akidai kwa wakati huo anasoma kidato cha pili.Miaka miwili ilikatika huku wawili hao wakiwa kwenye mapenzi, Abasi akijua kuwa ‘mtu’ wake anamalizia masomo.Hata hivyo, ilipofika siku ya matokeo ya kidato cha nne, Abasi aliomba kujua matokeo na kuhoji mbona haoni jina lake (Fatuma)!!
Ilidaiwa kuwa, Fatuma alimzuga kuwa alikatiza masomo dakika za mwisho hivyo dada yake akampeleka chuo.
Siku ya kupeleka posa ilipofika, Abasi alimuomba Fatuma ampeleke kwa wazazi wake, akamwambia awasiliane na dada yake, kumbe Fatuma alimpa dada feki ambaye aliongea na Abasi na kumwambia ampe siku mbili.
“Zilipita siku kama nne, tukamtafuta tena Fatuma na kumwambia aseme kama hataki ndoa kwani siku zinaenda na watu wameshajipanga na dada hajasema chochote, akajibu atatupeleka kwa shangazi yake ambaye anakaa Kigamboni (Dar).
Wakimeremeta
siku ya harusi yao. “Siku iliyofuata, akampeleka Abasi kwa shangazi
yake, uamuzi ukatoka kuwa mahari ipelekwe Mburahati (Dar) kwa shangazi
mwingine.“Mahari ilipelekwa ambapo walitaka shilingi laki saba,
zikatolewa shilingi laki tano kisha laki mbili tukaahidi kumalizia siku
ya ndoa.
njiani waliambiwa waende msikitini ingawa kuna watu waliokuwa wameshatangulia nyumbani, wakadai kuwa hakukuwa na dalili ya mtu kuonesha kuwa kuna sherehe.Walipofika msikitini, Mburahati walifunga ndoa ingawa shehe alitia shaka na kumuuliza Fatuma kama ni mjane kwani wapo watu waliomtonya kuwa ni mjane.
Fatuma alikana si mjane, ndoa ikafungwa kwa shaka huku shehe akiendelea kujiridhisha.
Fauzia alisema kuwa baada ya ndoa, watu walitimba Kigamboni kwa ajili ya sherehe ndipo baadhi ya waalikwa waliporopoka kwamba, Fatuma ana watoto wanne na ni mtalaka aliyeachwa siku sita zilizopita hivyo bado yupo eda.
Kikao cha familia kilipokaa, mume wa Fatuma (baadaye iligundulika jina lake ni Asha) wa kwanza aliyejulikana kwa jina moja la Masoud alifika na kukiri kuwa alimuoa Fatuma na amezaa naye watoto wanne.
Shehe
aliamuru kuvunjwa kwa ndoa ya Abasi na Fatuma ndipo bwana harusi
akazimia tena, alipoamka na kuuliza mkewe yuko wapi, akaambiwa
kilichotokea, akazimia tena.“Hali ya kuzimia ilitokea kama mara tatu na
mara ya mwisho alipoamka alikuwa bubu, tukalazimika kumwita shehe
amsomee dua ndipo akaanza kuongea,” alisema Fauzia.
Fauzia alisema harusi hiyo imewagharimu zaidi ya Sh. milioni 7 hivyo ni kitendo ambacho hawatakisahau na wanaomba watu waijue habari hii ili iwe fundisho kwa wengine.
Fauzia alisema harusi hiyo imewagharimu zaidi ya Sh. milioni 7 hivyo ni kitendo ambacho hawatakisahau na wanaomba watu waijue habari hii ili iwe fundisho kwa wengine.
0 comments:
Post a Comment