Hali imeendelea kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Mara, Ester Bulaya, kutangaza kukitosa kwa kutangaza uamuzi wake wa kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
Bulaya
 ambaye alikuwa mbunge machachari kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano 
wa Tanzania kuvunjwa na Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni , ametangaza 
kutogombea ubunge kupitia CCM wakati akizungumza na mtandao huu  baada 
ya kazi ya kuchukua fomu ndani ya chama hicho na kurejesha kuhitimishwa 
rasmi nchini jana.
Tangu
 mwanzo mwa mwaka huu, Bulaya alitangaza kugombea ubunge katika Jimbo la
 Bunda kupambana na Mbunge aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa 
Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.
Bulaya
 amekuwa kada wa pili ambaye alikuwa mbunge kutangaza kutogombea ubunge 
kwa tiketi ya CCM, mbunge wa kwanza kutangaza kutogombea ubunge  kupitia
 CCM baada ya James Lembeli, ambaye alikuwa Mbunge wa Kahama.
Hata
 hivyo, Bulaya hakuweka wazi kama ana mpango wa kuhamia chama kingine 
cha siasa na kutimiza azma yake ya kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu 
wa mwaka huu.
Ingawa
 Bulaya hajaweka wazi, vyama ambavyo vimekuwa vikitajwa kusubiri makada 
kutoka CCM kujiunga navyo ili wawanie ubunge ni Chama cha Demokrasia na 
Maendeleo (Chadema), ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (Cuf).
Mwenyekiti Monduli Apigilia Msumari
Wakati
 ikiwa hivyo kwa Bulaya, hali bado si shwari ndani ya CCM Wilaya ya 
Monduli baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Edward 
Sapunyo, Kupigilia msumari wa mwisho na kubariki hatua ya madiwani wake 
20 kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
 (Chadema).
Akizungumza
 mjini hapa jana, Sapunyo ambaye alikuwa Diwani wa kata ya Moita, 
alisema madiwani wake hawawezi kusubiri hadi Mbunge wa Jimbo la Monduli 
na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, atoe kauli kuhusu hatma yake 
ya kisiasa ndani ya CCM.
Kauli
 ya Sapunyo ambaye hatagombea udiwani uchaguzi wa mwaka huu, imekuja 
siku moja baada ya madiwani 20 wa jimbo hilo kutangaza rasmi kukihama 
chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
“Hatuwezi
 kuona baba yetu anapigwa na kuanguka chini halafu tusubiri kauli yake, 
ni lazima tuchukue hatua mara moja…hii haivumiliki, kitendo 
alichofanyiwa (Lowassa) na vikao vya CCM mjini Dodoma hivi karibuni kwa 
kukata jina lake pasipo kumpa haki ya kumsikiliza siyo cha 
kidemokrasia,” alisema.
Lowassa
 na makada wenzake wa CCM 38 walichukua fomu ya kuomba  ridhaa ya 
kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera ya kuwania kiti cha urais 
katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Katika
 kinyanyang’anyiro hicho, jina la Lowassa na wenzake yalikatwa katika 
hatua ya mwanzo, hali ambayo imezua malalamiko kwamba ikidaiwa kuwa 
hawakupewa
nafasi ya kuhojiwa.
“Tumepigwa,
 tumesambaratika (CCM) Monduli, hatuwezi kuchukua fomu za kuomba 
kugombea au kutetea nafasi zetu ndani ya chama hiki, tumehamia Chadema,”
 alisema.
Akizungumzia
 hali ilivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, alidai 
kuwa siyo kweli kwamba madiwani wote wamekihama chama chao.
Kimaro alidai kuwa baadhi ya madiwani waliotangaza kukihama chama hicho wameanza kusalitiana.
Alisema
 madiwani hao ambao anawaita ni makada baada ya Baraza la Madiwani la 
Halmashauri ya Monduli kuvunjwa, walifanya mkutano kwa kushawishiwa na 
mmoja wao.
Alisema
 ushawishi huo unatokana na uchu wa madaraka alionao kwa kuwa tayari 
wananchi wa Jimbo la Monduli, wanapenda aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum 
CCM, Namelok Sokoine, kuchukua fomu za ubunge wa jimbo hilo.
Alisema
 kutokana na ugumu huo, diwani huyo wa zamani ametumia mbinu ya 
kuwarubuni wenzake wakihame chama hicho ili agombea ubunge kwa tiketi ya
 Chadema.
“Huo ni uchu wa madaraka aliyo nayo,” alisema na kuongeza: “Diwani huyo hakubaliki na wananchi wa kata yake."
Alidai
 kabla ya kutangaza kukihakama chama hicho, madiwani hao walikuwa 
wameshafanya kikao na kuweka azimio la pamoja la kuondoka CCM, lakini 
juzi walipotangaza uamuzi wao, walijikuta wapo madiwani watatu.
Alisema
 baadhi ya madiwani walimfuata ofisini kwa lengo la kumuomba radhi 
lakini yeye aliwaambia waende kuwaomba radhi wananchi katika kata zao.
“Madiwani wachache walikuja hapa ofisini kuomba radhi kwa Katibu wa CCM Wilaya, nikawaambia waende kuwaomba radhi wananchi,” alisema.
Akimzungumzia
 Lowassa, alisema anachoelewa ni kwamba hajatoa tamko lolote kama 
anakihama chama hicho kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na mitandao ya 
kijamii.
“Bado
 tuna imani na Lowassa kuwa ni CCM, mpaka sasa hajatoa tamko lolote 
kukihama chama, lakini ikiwa vinginevyo itakuwa hatari kubwa,” alisema.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment