Chama
cha ACT Wazalendo kimesitisha rasmi uenyekiti wa aliyekuwa Mwenyekiti
wa chama hicho tangu kuanzishwa kwake, Anna Mghwira, baada ya kuteuliwa
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuazia jana Juni 7.
Uamuzi
huo umefanywa na kikao cha Kamati ya Uongozi ya chama hicho ambacho pia
kimemteua Mwenyekiti wa Kamati ya Mafunzo, Oganaizesheni na Uanachama
kuwa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho hadi uchaguzi mkuu utakapofanyika
mwezi Machi mwakani.
Akitangaza
uamuzi huo kwa wanahabari jana , Kaimu Kiongozi wa chama hicho, Samson
Mwigamba amesema sababu kuu ya kusitisha uenyekiti wa Anna Mghwira, ni
ili kumpa nafasi ya kutekeleza majukumu yake mapya aliyopewa na Rais wa
Tanzania, pamoja na kumfanya asiwe na mgongano wa kimaslahi ya kichama
wakati akitekeleza majumu yake kama kiongozi.
“Sisi
kama ACT hatupingi uamuzi wa mamlaka ya Rais, isipokuwa kamati ya
uongozi imeona ni busara kumpa nafasi Anna Mghwira kutumikia nafasi moja
kama kiongozi, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa ACT Wazalendo.
Kabla ya kutangaza uamuzi huo tayari tumewasiliana naye na tumekubaliana
hivyo. Tunamtakia kila la heri katika majukumu yake mapya,” alisema Ado Shaibu ambaye ni Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa umma.
Pamoja
na hayo Mwigamba alimpongeza Rais kwa kuvunja miiko ya siasa za
Tanzania kwa kumpatia mpinzani nafasi hiyo ndani ya serikali yake na
kuongeza kuwa kama chama hawana tatizo kwa kiongozi huyo kukabidhiwa
ilani ya CCM kwa sababu anakwenda kutumikia serikali kuu na Taifa.
0 comments:
Post a Comment