Wabunge
wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ambao
wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, watalipwa nusu mshahara na
posho zinazoambatana nao kwa miezi kumi.
Stahiki
hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya Bunge inayosema, “mbunge
aliyesimamishwa hataingia tena sehemu yoyote ya ukumbi na maeneo ya
Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa na atalipwa nusu mshahara
na nusu posho zinazoambatana na mshahara huo.”
Vilevile,
kutokana na uamuzi huo wabunge hao watakosa siku 65 za Bunge
zinazojumuisha siku 25 zilizobaki za Bunge la bajeti linaloendelea,
Bunge la Oktoba na lile la Februari, 2018. Vikao vya mabunge hayo
mawili; la Oktoba na Februari kila kimoja huwa na mikutano ya wiki mbili
mbili.
Wabunge
hao walisimamishwa juzi kwa azimio la Bunge licha ya kutokuwapo au
kujitetea kutokana na tuhuma zilizokuwa zinawakabili za kudharau kiti
cha spika.
“Tukutane Bunge lijalo la bajeti,” alisema juzi Spika wa Bunge, Job Ndugai. Bunge la bajeti huanza mwezi Aprili.
Kufikia
uamuzi huo, kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge ilisema
iliwatafuta kwa simu wabunge hao, lakini haikuwapata. Pia, iliwatumia
ujumbe mfupi ambao haukujibiwa na ilipowapelekea hati ya wito
haikuwakuta majumbani kwao.
Kwa
kutambua umuhimu wa agizo ililonalo na kuzingatia matakwa ya kisheria,
hati hizo ziliachwa baada ya kuelezwa kwamba wahusika hawapo kwani
wamesafiri. Baada ya jitihada hizo kushindwa kuzaa matunda, kamati
iliendelea kuwajadili bila wao kuwapo na kutoa maazimio hayo.
0 comments:
Post a Comment