For the Record: What Goes Around Comes Around!!!
Leo wapinzani wa Serikali ya Magufuli tumesemwa sana na kutishiwa kushughulikiwa bungeni na nje ya Bunge.
Kwa sababu hiyo, naomba niweke rekodi ya masuala haya sawa sawa.
Mwezi Machi '97 Bunge lilipitisha Sheria 2 kwa siku moja kwa kutumia Hati ya Dharura.
1)
Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbali mbali za Fedha ya '97 ilifuta au
kupunguza kodi nyingi kwa ajili ya makampuni ya kigeni ya madini.
2)
Sheria ya Uwekezaji Tanzania '97 iliwapa wawekezaji wa kigeni ulinzi
mkubwa na manufaa mengi kama vile kuondosha nje fedha na faida yote
wanayopata kwa uwekezaji wao nchini.
Mwaka
'98 Bunge lilipitisha Sheria ya Madini '98 ambayo ilitamka kwamba
mwenye milki ya madini na fedha yote itokanayo na mauzo ya madini ni
mwenye leseni ya kuchimba madini hayo.
Sheria
hizo tatu nimeziita 'Utatu Usio Mtakatifu' (Unholy Trinity) katika
maandiko yangu mbali mbali, na nimezichambua sana tangu mwaka '99
nilipoanza harakati dhidi ya sekta ya madini ya aina hii.
Kwa
miaka yote hii hadi leo, Sheria hizi za madini zimeungwa mkono na
kupigiwa debe na kila kiongozi na mbunge wa CCM, Magufuli included.
Watu
hawa, with very few and minor exceptions, ndio wamekuwa washangiliaji
wakubwa wa unyonyaji wa makampuni ya kigeni ya madini katika nchi yetu.
Na ukweli ni kwamba watu hawa na Chama chao ndio wamefaidika sana na utaratibu huu katika sekta ya madini.
Wachache
tuliopinga utaratibu huu tuliitwa kila aina ya majina mabaya na
uzalendo wetu ulihojiwa kama unavyohojiwa leo na Magufuli.
Kwa
mfano, Rais Mkapa alidai, wakati anazindua Mgodi wa Bulyanhulu, kwamba
upinzani wetu ulikuwa ni 'ujinga uliofichama katika kivuli cha taaluma.'
Baadhi
yetu, kama mimi na Dr. Rugemeleza Nshala, tulikamatwa na kushitakiwa
mahakamani kwa uchochezi. Tulikabiliwa na kesi hiyo kuanzia Mei '01 hadi
'08 ilipofutwa kwa kukosekana ushahidi.
Kama
ilivyokuwa wakati wa Mkapa mwaka '01, leo pia Rais Magufuli ametukebehi
na kuahidi kutushughulikia 'tukiropoka' nje ya Bunge.
Tunaambiwa
ni lazima tumuunge mkono Rais wetu katika hii 'vita ya uchumi.' Ni
sheria ipi ya Tanzania inayotulazimu kumuunga mkono Rais wetu hata kama
tunaona amekosea???
Hebu
naomba tuitafakari hii 'vita ya uchumi' kidogo. Je, nani hasa ni maadui
zetu katika 'vita' hii??? Ni makampuni ya madini ya kigeni??? Kama ni
hivyo, fikiria yafuatayo:
1)
Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake wameiruhusu Acacia
Mining (tunayoambiwa hata haijasajiliwa!!!) kuendelea kuchimba,
kusafisha na kusafirisha nje ya nchi dhahabu kutoka Bulyanhulu, Buzwagi
na North Mara Tarime.
Amezuia magwangala yasisafirishwe nje kwenye makontena lakini dhahabu yenyewe hamna shida ikisafirishwa na wezi hawa!!!!!
2)
Wakati mapambano ya 'vita ya uchumi' yakiendelea, dhahabu yote
inayochimbwa Geita Gold Mine (Mgodi mkubwa kuliko yote nchini)
inaendelea kuchimbwa, kusafishwa na kusafirishwa nje ya nchi.
3)
Wakati tuko vitani, Rais Magufuli na serikali yake ameruhusu kila mgodi
wa dhahabu nchini kuwa na kiwanja chake binafsi cha ndege ili wezi hawa
waweze kutorosha 'dhahabu yetu' kwa urahisi zaidi.
4)
Wakati tungali vitani, 'Utatu Usio Mtakatifu' wa sheria zetu za kodi,
uwekezaji na madini uko pale pale ulipokuwa mwaka '97-'98, cosmetic
changes excepted.
Aidha,
licha ya kuwa vitani, sisi bado ni signatories wa MIGA Convention na
bilateral investment treaties (BITs) zinazowalinda hawa tunaoaminishwa
kuwa ni wezi na maswahiba wao wa miaka yote.
5)
Wakati tuko kwenye hii vita kubwa ya uchumi, jemedari wetu mkuu na
serikali yake hawajatengua mkataba hata mmoja wa uendelezaji madini
(Mineral Development Agreements - MDAs) walizosaini hawa anaowaita
wanyonyaji na serikali za watangulizi wake Jakaya Kikwete na Ben Mkapa.
6)
Wakati tunahamasishwa kumuunga mkono jemedari huyu shupavu, bado
hatujaonyeshwa mkataba hata mmoja waliosaini na wanyonyaji hawa tangu
miaka ya mwanzo ya '90.
Leo Jemedari Mkuu ameahidi kwamba mikataba hiyo italetwa bungeni. Safi sana.
Lakini je, hii ni mara ya kwanza tunaahidiwa hayo???
Mwaka '08 Jemedari Mkuu wa kabla yake alituahidi hivyo hivyo. Tuwe na subira kabla ya kuanza kushangilia prematurely.
7) Nimemsikia Magufuli akielekeza wahusika wote wa uchafu huu washughulikiwe. Kweli???
(a) Je, Jakaya Kikwete aliyesaini leseni za Bulyanhulu na Nzega mwaka '94 anaponaje???
(b) Je, Ben Mkapa aliyekuwa Rais na Mwenyekiti wa Cabinet wakati haya yanafanyika anaachwaje???
(c) Je, waliokuwa mawaziri na manaibu wao wote wakati haya yanatokea wanasalimikaje???
(d)
Je, wale washangiliaji na wapiga meza wa bungeni, ambao waliunga mkono
kila walicholetewa bungeni na kukipitisha kilivyo wanakosaje lawama???
8)
Nimesikia Acacia Mining hawana hata leseni/usajili wa kuendeshea
shughuli zao hapa nchini. Labda. Hata hivyo, jiulize yafuatayo:
(a)
Hivi wamekuwa wanalipa kodi kama PAYE, SDL, income tax, withholding
tax, mrahaba, n.k., kwa kutumia jina gani miaka yote hii???
(b) Je, wana akaunti yoyote katika benki za Tanzania??? Kama ndio, wamezifungua kwa jina gani???
Kama hapana, wanalipaje mishahara ya wafanyakazi wao wa Kitanzania au watoa huduma mbali mbali wa Kitanzania???
(c) Je, wanalipa bili za umeme kwa TANESCO au za simu kwa Vodacom, Tigo, Airtel, n.k. kwa kutumia jina gani???
(d) Je, wamesajiliwaje katika Soko la Hisa la Dar kama Acacia kama wanaendesha shughuli zao kihuni hivi???
(e)
Kuna kitu kinaitwa 'estoppel' katika Sheria yetu ya Mikataba (the Law
of Contract Act, Cap. 345) na katika Sheria yetu ya Ushahidi (the Law of
Evidence, Cap. 6).
Je, estoppel haituhusu kwenye suala hili la leseni au usajili ya Acacia???
Kama estoppel inahusika, je, hoja hii ya ukosefu wa usajili ina uzito gani, kama upo, kisheria???
9) Nimesikia Sheria za Madini zinatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa. Sawa kabisa.
Lakini
je, kwanini Rais Magufuli hajasema chochote juu ya Sheria za Gesi
Asilia na Mafuta ambazo zilipitishwa haraka haraka kwa Hati ya Dharura
baada ya sisi 'waropokaji' kutimuliwa bungeni na Spika Anna Makinda
mwaka '15???
Au
Rais wetu anaamini kwamba Sheria za Gesi Asilia na Mafuta hazina
matatizo licha ya kupitishwa kwa utaratibu ule ule uliotumika kwa Sheria
za Madini???
10) Wakati tunaingojea kwa hamu mikataba ya madini iletwe bungeni, hebu na tujiulize yafuatayo:
(a) Mikataba ya uchimbaji gesi asilia na mafuta nayo iko wapi???
(b)
Mikataba ya manunuzi ya Bombardier na Dreamliner za Magufuli nayo
italetwa bungeni au itabidi tusubiri aondoke madarakani kwanza kama
ilivyokuwa kwa JK na BM???
(c)
Mikataba ya ujenzi wa airport Chato na Reli ya Standard Geji ya
Waturuki au Wachina na mabarabara kibao nayo italetwa bungeni au ndio
basi tena tusubiri Bwana mkubwa atakapoondoka madarakani???
Wakati
tukisubiri kufukuzwa bungeni na Spika Ndugai kwa maelekezo ya bosi
wake, na wakati tukisubiri dhahama ya Bwana Mkubwa nje ya Bunge, hebu na
tujiulize hivi nani hasa ndiye mzalendo wa kweli wa nchi hii???
Hebu
na atutajie majina na namba za simu za wale wote ambao amedai wamekuwa
wanawasiliana na Acacia na lini walifanya mawasiliano hayo na yalihusu
kitu gani. Kutoa hukumu kwa innuendo peke yake haitoshi, tunahitaji
ushahidi thabiti kutoka kwa Rais Magufuli.
Sijazungumzia
bado plagiarism ya taarifa mbali mbali za kiserikali na zisizo za
kiserikali katika Taarifa ya Kamati ya Prof. Osoro. Hili ni la baadae.
0 comments:
Post a Comment