Mwanasheria
Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco (54)
amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka matatu ya
kuishi na kufanya kazi nchini bila kuwa na kibali.
Mwendesha Mashtaka wa Uhamiaji, Novatus Mlay alimemsomea mashtaka hayo leo Jumatano kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.
Akisoma
hati ya mashtaka, Mlay alidai kuwa Mei 19, 2017 huko Kinondoni
katika ofisi ya uhamiaji, Marco akiwa raia wa Burundi alikutwa nchini
bila kuwa na kibali cha kumuwezesha kuishi.
Marco
katika shtaka la pili amedaiwa kuwa siku hiyo alikutwa akifanya kazi
kama Mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu
kufanya kazi hapa nchini.
Katika
shtaka la tatu, Mlay alidai kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya
Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo Wilaya ya Ilala, mshtakiwa huyo akiwa
raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi
wakati akijaza fomu ya kuomba hati ya kusafiria namba CT (5)(Ai).
Wakili
Mlay alisema kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha
Marco kupata hati ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku
akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Mshtakiwa
alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika ambao kila mmoja
atasaini bondi ya Sh 20 milioni na alikamilisha. Kesi imeahirishwa hadi
Juni 21, 2017 kwa ajili ya kutajwa.
0 comments:
Post a Comment