Filamu ya Wema Sepetu na muigizaji wa Ghana, Van Vicker ‘Day After
Death’ inatarajiwa kuzinduliwa September mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Wema ameiambia Mpekuzi kuwa Van Vicker atakaa kwa wiki mbili zaidi
kwaajili ya kufanya filamu nyingi na muigizaji huyo
aliyeibuka na tuzo ya muigizaji wa kike anayependwa kwenye tuzo za watu
zilizotolewa Ijumaa iliyopita.
“Tunaplan kuilaunch movie yetu mwezi wa tisa, kaniambia kwamba akija
he is going to stay for another two weeks na anategemea tutafanya shoot
nyingine huku huku,” amesema Wema.
Wema amedai amefurahia kufanya kazi na Van Vicker ambaye jana alimpongeza kwa ushindi wake wa tuzo za watu.
“Congrats @wemasepetu on your award for ‘Best & Loved’ Actress
2015. You deserve it. #DayAfterDeath our movie together should take you
another notch higher. Thanks for trusting me. #HatsOff4U
#TheYoungGodFather #TheEntrepreneur #TheVanVickerBrand,” aliandika Van
kwenye Instagram.
0 comments:
Post a Comment