Mzuka wa siasa unazidi kuwaingia wasanii wengi wa muziki nchini. Keisha ni mmoja wao.
Akizungumza na Mpekuzi, Keisha amesema naye pia ana mpango wa kuingia
rasmi kwenye kuwania nafasi ya uongozi wa kisiasa japo inaweza isiwe
mwaka huu.
“Napenda sana harakati za siasa, nimeshawahi kufikiria lakini bado
sikupata jibu sahihi,” amesema.
“Kwahiyo sasa hivi siwezi kusema nipo
tayari ama vipi. Lakini nikiwa tayari nitaweka wazi kila kitu. Mimi ni
mwana-CCM damu kabisa nimekunywa maji ya bendera.”
Miongoni mwa wasanii watakaogombea ubunge mwaka huu ni pamoja na Profesa Jay na Afande Selle.
0 comments:
Post a Comment