Ni nadra sana kukutana na Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi maarufu kama 
K-Lynn lakini kupitia tuzo za watu tulifanikiwa kupiga story mbili tatu.
K-Lynn ameiambia Bongo5 kuwa maisha akiwa kama mama watoto wawili mapacha yamekuwa ya aina yake na anayafurahia kila sekunde.
“Nimejifunza kuwa mvumilivu, nimejifunza upendo ambao sijawahi 
kujisikia kabla. Jinsi unavyompenda mtoto ni tofauti ambavyo unaweza 
kumpenda mtu yoyote yule katika maisha yako,” alisema.
Katika hatua nyingine Miss Tanzania huyo wa zamani alisema hakuna uwezekano wowote wa yeye kurejea tena kwenye muziki.
“Kwa bahati nzuri sana baada ya kufanya uamuzi wa kutokuwa kwenye 
muziki, niliweza kupata kitu kingine ambacho kimeuteka moyo wangu. 
Kufanya interior design kunanifurahisha kuliko hata muziki. 
"Nafurahi 
sana kujua kwamba kuna watu wangependa kunisikia ama kusikia nikiimba 
lakini nafikiri moyo wangu umehamia kwenye sanaa nyingine.”

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment