Siku
 zote mapenzi huyapa maisha thamani lakini wapo ambao hujikuta kwa namna
 moja ama nyingine wanatengana na wapenzi wao kwa sababu tu ya 
mihangaiko ya kila siku yakujitafutia ridhiki, masomo na wakati mwingine
 utengano huwa ni matokeo ya wapendanao kuishi sehumu tofauti hii 
huwakumba sana wanafunzi wa vyuo na shule za bweni.
Umbali
 hulifanya penzi baina ya wapendanao kuteteleka kama wapendanao 
hawatafanya kazi za ziada kuhakikisha wanaziba mianya yote 
itakayosababisha usaliti kama sio kuachana kabisa.i.Hata hivyo, mapenzi 
ya mbali huna ni vigumu kuteteleka endapo tu wapendanao wanamapenzi ya 
dhati na kutamani kuwa pamoja kila wakati na mmoja wapo kuamua kujitoa 
muhanga kwa kuamia anakoishi ama kufanyia kazi la azizi wake. Hata 
hivyo, mnaweza kudumisha mapenzi yenu ya mbali endapo utafanya haya:- 
Mawasiliano ya mara kwa maraMawasiliano
 ni nguzo muhimu sana baina ya wapendanao, humfanya kila mtu kuhisi 
uwepo wa mwenzi wake hata kama atakuwa mbali naye. Hivyo, kama una 
mpenzi wako aliye mbali nawe hakikisha unakuwa naye karibu kwa kumtumia 
ama sms, email, kadi au simu.
Aidha,
 pindi mnapowasiliana hakikisha humkwazi mwenzako kwa namna yoyote ile, 
kwani kuna watu wengi wanatabia ya kudharau baadhi ya mambo kutokana na 
kutingwa na shughuli kadha wa kadha, naomba nikuweke wazi kuwa hata kama
 umebanwa vipi pindi mpenzi wako aliyembali anapokutumia ujumbe kwenye 
simu yako basi usisite kumjibu katika muda muafaka na siyo kuuchuna hadi
 ulalamikiwe!
Heshimu hisia zakoMapenzi
 ya kweli yametawaliwa na hisia kali ambazo ndizo huwafanya wapendanao 
kufikishana kwenye mambo fulani kwani pasipo hisia hata uwe na ujuzi au 
utundu wakutosha hutapata raha ya mapenzi.
Kama
 kweli unampenda kwa dhati mwenza wako na mmetengana kutokana na sababu 
za kimasomo ama kazi kwa hakika utakuwa tayari kumtunzia penzi lake hadi
 mtakapokutana tena.
Uaminifu
 pekee ndio utakaokufanya uwasiliane mara kwa mara na mwenza wako na 
kwenye uaminifu mapenzi hushamiri huku kila mmoja akimuonea wivu wa hapa
 na pale mwenzi wake, lakini sio ule wakubomoa! Hivyo heshimu hisia zako
 kama kweli unampenda mwenzi wako kwa kumuonyeshe unampenda.
Umbali si kigezo cha kunyimanaMpe
 mwandani wako raha kamili kama ilivyokuwa awali mlipokuwa pamoja! Bila 
shaka unajiuliza inawezekanaje? Hili linawezekana kwa kutumia njia 
yoyote ya mawasiliano. Mfano kama nyote mna simu jiandaye vyakutosha 
nikiwa na maana uhakikishe upo sehemu ambayo utakuwa huru kuongea ama 
kufanya chochote kitakachokufanya uhisi raha isiyo na kifani na 
kukufikisha kwenye kilele cha mlima kilimanjaro bila kutarajia.

Bila
 shaka kila mtu anamfahamu vema mpenzi wake na hasa nini hupenda 
kufanyiwa ili aweze kufika safari yake na kama ndivyo basi hakikisha 
unafanya mambo yote ambayo ukimfanyia mwenzi wako pindi mnapokuwa kwenye
 mambo fulani hupagawa.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment