Pages

Ads 468x60px

Friday, May 29, 2015

MWANAFUNZI WA MIAKA 15 ABAKWA NA KUPEWA MIMBA, CHA AJABU WAZAZI WA MWANAFUNZI WASHIRIKI KUMFICHA MTUHUMIWA

Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kihanda wilaya ya Karagwe mkoani Kagera mwenye umri wa miaka 15 aliyetekwa nyara na kufichwa porini miezi mitatu amerejea nyumbani kwao akiwa mjamzito huku akiomba msaada kwa watendaji wa serikali wamdhibiti baba yake mzazi anayetaka kumuozesha kwa nguvu kwa lengo la kujipatia mahali ya shilingi milioni saba na Ng’ombe kumi wakidai kuwa amepoteza sifa za kuendelea na masomo.

Akizungumza binti huyo ameelezea jinsi alivyotekwa nyara akiwa njiani kwenda shule kujisomea masomo ya ziada.
 
Kwa upandewake kaka wa binti huyo Bw.Emmanuel John amebainisha ukweli wa mambo juu ya biashara haramu inayofanyika kumuozesha mdogo wake katika familia ya wafugaji inayodaiwa kusambaza fedha kwa njia za rushwa ili mtuhumiwa Bw.David Kapipi asikamatwe kwa kosa la kubaka na kusababisha ujauzito mwanafunzi wa kidato cha pili.
 
Baada ya majibu hayo chombo hiki kilifika nyumbani kwao mtuhumiwa Bw.David Kapipi mkazi wa kijiji cha Mabale wilaya ya Misenyi mkoani Kagera ambaye hakuwepo ila ndugu zake wakizungumza kwa mashariti ya kutopigwa picha walisema kuwa jambo hilo lipo kwenye mazungumzo ya wazazi wa pande zote mbili ambapo mzee Kapipi alipopigiwa simu ikawa hivi.
 
Akizunzumza kwa sharti la kutopigwa picha mkuu wa polisi wilaya ya Karagwe Bw.Mika Makanja amesema polisi inamtafuta mtuhumiwa na kusema kwamba waandishi watakapo muona mtuhumiwa waisaidie polisi kumkamata na umfikisha kituo cha polisi achukuliwe hatua za kisheria
 

Chanzo: ITV 

0 comments:

Post a Comment

SHARE