Mwanafunzi
 wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kihanda wilaya ya Karagwe 
mkoani Kagera mwenye umri wa miaka 15 aliyetekwa nyara na kufichwa 
porini miezi mitatu amerejea nyumbani kwao akiwa mjamzito huku akiomba 
msaada kwa watendaji wa serikali wamdhibiti baba yake mzazi anayetaka 
kumuozesha kwa nguvu kwa lengo la kujipatia mahali ya shilingi milioni 
saba na Ng’ombe kumi wakidai kuwa amepoteza sifa za kuendelea na masomo.
Akizungumza binti huyo ameelezea jinsi alivyotekwa nyara akiwa njiani kwenda shule kujisomea masomo ya ziada.
Kwa
 upandewake kaka wa binti huyo Bw.Emmanuel John amebainisha ukweli wa 
mambo juu ya biashara haramu inayofanyika kumuozesha mdogo wake katika 
familia ya wafugaji inayodaiwa kusambaza fedha kwa njia za rushwa ili 
mtuhumiwa Bw.David Kapipi asikamatwe kwa kosa la kubaka na kusababisha 
ujauzito mwanafunzi wa kidato cha pili.
Baada
 ya majibu hayo chombo hiki kilifika nyumbani kwao mtuhumiwa Bw.David 
Kapipi mkazi wa kijiji cha Mabale wilaya ya Misenyi mkoani Kagera ambaye
 hakuwepo ila ndugu zake wakizungumza kwa mashariti ya kutopigwa picha 
walisema kuwa jambo hilo lipo kwenye mazungumzo ya wazazi wa pande zote 
mbili ambapo mzee Kapipi alipopigiwa simu ikawa hivi.
Akizunzumza
 kwa sharti la kutopigwa picha mkuu wa polisi wilaya ya Karagwe Bw.Mika 
Makanja amesema polisi inamtafuta mtuhumiwa na kusema kwamba waandishi 
watakapo muona mtuhumiwa waisaidie polisi kumkamata na umfikisha kituo 
cha polisi achukuliwe hatua za kisheria
Chanzo: ITV 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment