JESHI la Polisi Mkoa wa Rukwa, linawashikilia askari polisi wawili kwa tuhuma za kuiba bunduki aina ya SMG mali ya jeshi hilo.
Akizungumza
mjini hapa jana, Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Rukwa, Leons
Rwegasira, alisema bunduki hiyo iliibwa Mei 19 mwaka huu katika Kituo
cha Polisi mjini Namanyere, Wilaya ya Nkasi.
Pamoja
na kuthibitisha wizi huo, Kamanda Rwegasira hakutaka kutaja majina ya
watuhumiwa kwa kile alichosema kuwa uchunguzi bado unaendelea.
“Kuna
polisi wawili tunawashikilia kwa tuhuma za wizi wa bunduki na upotevu
huo uligunduliwa Mei 19 mwaka huu baada ya ukaguzi wa kawaida kituoni
hapo kufanyika.
“Baada
ya upotevu wa silaha hiyo kuwapo, msako mkali ulianza mara moja na
hatimaye silaha hiyo ilipatikana ikiwa imefukiwa chini ya ardhi.
“Kwa
hiyo, watuhumiwa bado tunaendelea kuwashikilia huku upelelezi
ukiendelea na utakapokamilika, tunaweza kuwafikisha mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake,” alisema Kamanda Rwegasira.
0 comments:
Post a Comment