Jeshi la Polisi limekanusha madai ya polisi wa wilaya ya Bunda, wanaodai kulazimishwa kuchangia fedha kwa ajili ya mafuta ya kusafirisha mwili wa mwenzao aliyefariki dunia katika Hospitali ya rufaa Bugando kwenda nyumbani kwao katika wilaya ya Mahenge mkoani Morogoro.
Jeshi limetoa kauli hiyo baada ya kuwapo malalamiko katika Kituo
Kikuu cha Polisi cha Wilaya ya Bunda, ambako kulikuwa na umati mkubwa wa
askari Polisi waliokuwa wamekusanyika, wakidai kupinga amri ya
kulazimisha kuchanga fedha kwa ajili ya kusafirisha mwili wa mwenzao.
Baada ya mwandishi kusikiliza malalamiko ya polisi hao, alizungumza
na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya (OCD), Gwisael, ambaye alikanusha
kuhusu madai ya askari hao.
Alisema, mchango wanaotoa ni wa Sh 5,000 kama ilivyo kawaida na siyo za mafuta Sh 10,000, kama inavyodaiwa na baadhi ya askari.
Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Philipo Kalangi, alimwambia
mwandishi kwamba, imetolewa gari na mafuta lita 220 kwa ajili ya
kusafirisha mwili wa askari huyo, Koplo Mahamudu Magasa.
Kamanda Kalangi alisema ni marufuku kwa askari yeyote kuchangishwa
mchango wa mafuta.
“Tayari nimeshatoa gari na mafuta lita 220 kwa ajili ya kusafirisha mwili wa askari huyo, na pia tunatoa na posho ya kujikimu kwa askari watakaosafirisha mwili wa marehemu, sasa ni nani kawaambia wachangie tena…sisi tuna utaratibu wetu wa serikali siyo kuchangisha askari fedha za mafuta,” alisema.
“Tayari nimeshatoa gari na mafuta lita 220 kwa ajili ya kusafirisha mwili wa askari huyo, na pia tunatoa na posho ya kujikimu kwa askari watakaosafirisha mwili wa marehemu, sasa ni nani kawaambia wachangie tena…sisi tuna utaratibu wetu wa serikali siyo kuchangisha askari fedha za mafuta,” alisema.
Hata hivyo, jana saa 7:52 mchana, mwandishi alishuhudia gari la
Polisi lililotumwa na Kamanda wa Mkoa kutoka mjini Musoma, lenye namba
za usajili DFP 1822 likiwa tayari liko kituoni hapo kusubiri kusafirisha
kwa mwili wa marehemu.
Askari huyo, Mahamudu aliugua juzi na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa
Bugando jijini Mwanza ambako alifariki dunia. Awali, askari waliokutwa
kituo cha Polisi wakilalamikia kuchangishwa, walisema kitendo hicho ni
sawa na kwamba serikali haithamini utumishi wao.
Walidai watumishi wa idara nyingine wanapofariki fedha hutolewa na
serikali kwa ajili ya kusafirisha miili yao. “Iweje sisi tulazimishwe
kuchangia,” alihoji mmoja wa askari.
Walisema kuwa wao siku zote wamekuwa wamejiwekea utaratibu, kwamba
mwenzao anapofariki wanachangia mchango wa Sh 5,000 kila mmoja, zisaidie
familia ya marehemu na siyo kuchangia mafuta ya kusafirisha mwili wa
marehemu.
Hata hivyo, wakati polisi hao wakiwa wamekusanyika nje ya kituo hicho
wakipinga hatua hiyo, maofisa wa jeshi hilo wilayani hapa wakiongozwa
na Mkuu wa Polisi katika wilaya ya Bunda, walikuwa kwenye kikao cha
pamoja.
0 comments:
Post a Comment