NAIBU
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salim
Mwalim, amesema Profesa Mark Mwandosya, ajiunge na Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) ili awe mshauri kuliko kuendelea kuwepo CCM.
Akizungumza
jana kwenye mkutano wa hadhara aliofanya katika Jimbo la Rungwe
Mashariki linaloongozwa na Mwandosya, alisema CCM imekosa mwelekeo hivyo
msomi kama Mwandosya hatakiwi kuwa katika chama hicho.
Alisema
japo mbunge huyo alisema hatagombea tena jimbo hilo la Rungwe
Mashariki, kinachotakiwa ni kukihama chama hicho na kujiunga na Ukawa
ili awe mshauri wa Umoja huo.
“Mwandosya
ni msomi mkubwa sana hivyo kutokana na elimu yake aliyonayo, anatakiwa
kutoka CCM na kujiunga na Ukawa ili awe mshauri wetu na sio kuendelea
kubaki na CCM,” alisema Mwalim.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mbeya, Joseph China, alisema
wananchi wanatakiwa kujiandikisha ili kuweza kupata haki yao ya msingi
ya kupiga kura.
China alisema njia pekee ya kuweza kuishinda CCM ni wananchi kujiandikisha kwa wingi na kuhudhuria siku ya kupiga kura.
Alisema
katika kata hiyo ya Kandete kumekuwepo na tatizo la kutokuwepo kwa
diwani hivyo michango imekuwa ikichangishwa kiholela na watendaji wa
vijiji na kata bila kujua matumizi ya hizo fedha.
0 comments:
Post a Comment