Pages

Ads 468x60px

Monday, June 15, 2015

Rais Bashir wa Sudan aondoka Afrika Kusini pamoja na kuzuiwa na Mahakama>>SOMA HAPA



Omar Al Bashir, Rais wa Sudan ameripotiwa kuondoka Afrika Kusini pamoja na kuwepo kwa amri ya mahakama ya nchi hiyo kumzuia kuondoka.

Awali ndege ya Al Bashir iliripotiwa kuwa ilikuwa imetoweka katika kiwanja cha ndege Johannesburg na kuhamishiwa katika kiwanja cha jeshi nchini humo.

Tayari mtandao wa habari wa AFP umeripoti kuwa Rais Bashir ameshatua mjini Khartoum, Sudan.

Walipoulizwa juu ya Bashir, maafisa wa Wizara ya sheria ya Afrika Kusini wamedai kuwa hawajui Rais huyo alipo.

Mapema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon alikuwa amesistiza kuwa amri ya mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC lazima iheshimiwe na Afrika Kusini.
Ndege inayosadikiwa kuwa ya Rais Omar Bashir wa Sudan ikiruka kutoka uwanja mmoja wa ndege karibu na mji wa Preatoria, nchini Afrika Kusini

Kuondoka kwa Bashir kumekuja kabla ya uamuzi rasmi wa mahakama wa kama akamatwe au la.

0 comments:

Post a Comment

SHARE