Pages

Ads 468x60px

Monday, June 15, 2015

Wanawake Washauriwa Kuepuka Rushwa ya NGONO Kwenye Uchaguzi>>soma hapa!!



Wanawake nchini wametakiwa kuacha kutumia rushwa ya ngono ili waweze kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi bali watumie uwezo wao kupambana ili waweze kushika nafasi za juu kwenye ngazi za maamuzi.

Hayo yalibainishwa na aliyekuwa mbuge wa Ukerewe (CCM), Balozi Getruda Mongela (pichani), wakati alipokuwa akifungua kongamano la kitaifa la wanawake mjini Dodoma.

Alisema mwanamke anayetumia ngono ili aweze kuchaguliwa katika uchaguzi hafai kuongoza na jamii haina budi kumwogopa.

“Mwanamke ambaye anatumia rushwa ya ngono ili kupata uongozi huyo ni mwasherati na hapaswi kuaminiwa katika kupewa nafasi yeyote ya madaraka katika serikali yoyote ile,” alisema Mongela.

Aidha, alisema kuwa katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu wanawake wanatakiwa kuwa kitu kimoja bila kujali itikadi zao za vyama kwani wao ndiyo wamekuwa wakipata shida katika kutafuta huduma mbalimbali za kijamii.

“Mimi nikiwa Chadema na wewe CCM lakini mwisho wa siku tunakutana hospitali ili kuweza kujifungua tukiwa wodi moja hivyo basi sisi tuwe na ajenda yetu moja kama wanawake,” alisema.

Alisema kuwa pia wanawake wanatakiwa kuachana na imani za kishirikina katika uchaguzi ujao kwa kuwa haiwezi kuwasaidia hata kidogo kuingia madarakani bali wawe karibu na wananchi na kupanga sera zao zenye tija.

“Kama uchawi ungekuwa unauwezo huo basi wale waganga wa kienyeji wao kwanza wangekuwa wabunge unafikiri kwani wao hawapendi kuwa wabunge?” alihoji. 
 
Hata hivyo, aliwataka wanawake kuwa na tabia ya kuthubutu katika kufanya maamuzi yao na kuweka uwoga pembeni kwa kuwa hiyo ndiyo itakuwa silaha yao katika kupata nafasi za juu za uongozi.

0 comments:

Post a Comment

SHARE