Pages

Ads 468x60px

Monday, June 8, 2015

TARIME: Mwenyekiti CHADEMA mbaroni Akidaiwa kuiba Mlingoti wa bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)>>>>>>>>>>


MWENYEKITI wa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kijiji cha Sokini mji mdogo wa Sirari wilayani Tarime, Denisoni Makanya (44),  amepandishwa kizimbani mbele ya Hakimu, Gibogo Wenje, akidaiwa kuiba mlingoti wa bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wenye thamani ya Sh 80,000.

Mwendesha Mashtaka wa Oolisi, George Lutonja, alidai  mshtakiwa  alitenda kosa hilo usiku Mei 29, mwaka huu.

Mshitakiwa alikana shitaka na yuko nje kwa dhamana hadi Agosti 4 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

0 comments:

Post a Comment

SHARE