Pages

Ads 468x60px

Monday, June 8, 2015

SHINYANGA :CRDB yasaidia madawati>>>



BENKI ya  CRDB Shinyanga imetoa madawati 100 katika Shule ya Msingi Mwenge yenye thamani  ya Sh milioni 10  kuisaidia Serikali kupambana na changamoto ya uhaba wa madawati, anaripoti Kadama Malunde.

Msaada huo ulikabidhiwa juzi na Meneja wa Benki ya CRDB, Tawi la Shinyanga,  Saidi Pamui kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro katika shule hiyo yenye wanafunzi 1180.

0 comments:

Post a Comment

SHARE