Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta |
KWA UFUPI
Geita: Waziri
wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anasimama kifua mbele kupambana na
rushwa kwa kuwa aliwahi kuikataa rushwa ya Dola 70,000 (sawa na
Sh140,000) milioni).
Sitta alisema hayo
jana wakati akizungumza na makada wa chama hicho waliojitokeza
kumdhamini katika wilaya ya Geita mkoani Geita na kusema kuna baadhi ya
watia nia wanaopita wakisema kuwa wakiwa marais watapambana na rushwa
wakati ukiwatazama macho yao yanaonyesha ni wala rushwa. Viwango vya
kubadili fedha za kigeni, kwa sasa Dola moja ya Marekani sawa na
Sh2,000.
“Nilitumwa Canada
kutafuta ndege tatu, jioni moja tukiwa Canada tunajiandaa kuondoka,
akaja mkurugenzi wa masoko wa kampuni tuliyonunua ndege, akaniambia
waziri tuna kautaratibu hapa ukifanikisha ndege zetu zikanunuliwa
tunatoa bakshishi ya Dola 70,000 utataka hizi hela tuzipeleke benki
gani,” alisema Sitta akimnukuu ofisa huyo wa masoko.
“Watazameni hawa
watu... mtu kawa waziri mwaka mmoja leo anataka urais, halafu anasema
atapambana na rushwa…utapambana na rushwa wapi wakati hata hujapita
kwenye mitego ya rushwa. Watazameni kwa makini, mtawajua tu kwa macho,
kwani macho yao yamekaa kijanjajanja kweli,” alisema. Aliendelea, “Kwa
kuwa mimi nililelewa vizuri nilijua tu huo ni mtego wa shetani,
nikamwambia mkurugenzi nitampa jibu kesho, nikawasiliana na wakubwa
zangu kwanza wakakubali ni chukue hiyo pesa ikasomeshe marubani wa
ndege.”
Sitta aliwataka
wananchi hao kuwatazama kwa makini watangaza nia hao, na kuwauliza iwapo
tayari walishawahi kupambanishwa na rushwa.
Lowassa aonya kuhusu viongozi wanafiki
Kigoma. Wakazi wa
Kigoma wametakiwa kuwa makini na kauli za baadhi ya viongozi wa Serikali
wanaojinadi kwa kusema wanawapenda Watanzania maskini, lakini mioyoni
mwao hawana huruma.
Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa alipokuwa akitafuta wadhamini
mkoani hapa, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu zenye majina ya wanachama waliojitokeza kumdhamini.
Akiwa katika ofisi
ya CCM mkoa, Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Nohoji Kubaji
alimkabidhi Lowassa fomu 45 za wana CCM waliomdhamini.
“Wapo viongozi,
wanajifanya wanawapenda na kuwajali watu masikini, lakini wao wenyewe
unawakuta ni matajiri, hawa jamaa ni waongo sana hawa,” alisema.
Lowassa aliwataka
wakazi Kigoma kumuombea ili dua na sala zao ziweze kumsaidia afikie
malengo aliyojiwekea. “Nina dhamira ya kuwatumikia, lakini lazima
mniombee sana dua na sala ili mambo yangu yaende vizuri hatimaye
nishinde kuwa Rais wa Tanzania. Mimi nachukia sana umaskini, kwa hiyo
lazima tuwe kama Malaysia ambayo kiongozi wake alipambana kuhakikisha
wananchi wanaondokana na umaskini,” alisema.
Wasira awashangaa wanaotumia matarumbeta
Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika, Stephen Wasira amesema anashangazwa na baadhi ya
wagombea wenzake, wanaokwenda kutafuta wadhamini kwa matarumbeta na
miziki ya kuwaita wananchi.
Wasira alitoa kauli
hiyo mjini Musoma katika Ofisi ya CCM Mkoa, Adamu Ngalawa wakati
alipokuwa akipokea majina na kadi za wadhamini waliojitokeza kumdhamini.
Alisema wagombea
wanaofanya hivyo wanakiuka taratibu, kanuni, sheria na katiba za chama
kwa kuwa chama hicho tawala kilishapitisha kuwa wakati wa kutafuta
wadhamini hakuna mgomWbea kuhutubia mkutano wa hadhara.
“Kuna wagombea
wanaitisha mkutano wa hadhara na kuwaita wananchi wakati hawana cha
kuwahutubia kwa kuwa wamezuiliwa kufanya hivyo…wanabaki wakiwaeleza
wananchi mniombee, wawaombee nini? Mimi nimeshatembea mikoa zaidi ya 20
na hakuna sehemu nimewaita wananchi tofauti na kutoa taarifa kwenye
chama ili wadhamini niwapate,” alisema.
Wasira alisema mkoa
wa Mara una wagombea wanne wanaowania urais, lakini hakuna atakayejitoa
kwa misingi ya kuachiana kura kwa sababu hakuna mwananchi wa kawaida
atakayepiga kura bali maamuzi yatafanywa na Kamati Kuu ya CCM.
0 comments:
Post a Comment