KUFUATIA
taarifa iliyotolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee kuhusu utoaji wa ardhi kwa bilionea
Alhaji Aliko Dangote, wakazi wa kijiji cha Mgao, Halmashauri ya Mtwara
Vijijini wamemtaka kufuta kauli yake.
Wakitoa
malalamiko yao kwa vyombo vya habari, baadhi ya wakazi wa kijiji hicho
ambao walijitambulisha kwa majina ya Seif Said na Mohamed Njiti,
walisema kuwa kitendo cha ardhi yao kulinganishwa na kaniki na kipande
cha kanga kimewasikitisha.
Walisema
uthamini wa ardhi umeshaanza, wanatarajia kulipwa Sh milioni 10 kwa
ekari moja, huku wakipata malipo ya mimea iliyopo kwenye mashamba yao,
zoezi ambalo bado linaendelea katika maeneo ya vijiji vya Kisiwa na
Mgao.
Kwa
upade wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abdulahman Shaha, alisema
amesikitishwa na taarifa iliyotolewa kwa kulinganisha ardhi yao na
kipande cha kaniki.
“Ile
kauli sio sahihi, ilibidi aje Mgao apate taarifa sahihi ili akatoe
bungeni, sisi tuko katika tathmini ya ardhi, kila mwananchi atalipwa
stahiki yake, walipaji wa ardhi hii ni Mamlaka ya Bandari Tanzania siyo
Dangote,” alisema Shaha.
Naye
Meneja wa Mamlaka ya Bandari Mkoa wa Mtwara, Hebel Mwasenga, alisema
mamlaka hiyo inamiliki eneo la hekta 1,000, ambapo mwekezaji huyo
amepewa eneo la hekta 25 kwa ajili ya ujenzi wa bandari ndogo.
0 comments:
Post a Comment