Pages

Ads 468x60px

Monday, July 20, 2015

Wananchi Wampokea Magufuli Kwa Kishindo Mkoani Geita.>>



Mkoa wa geita na viunga vyake jana ulizizima kwa muda wakati mgombea wa kiti cha urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk.John Pombe Magufuli alipokuwa akitambulishwa na kuagwa na wapigakura wake wa jimbo  la Geita huku wananchi wakimtaja kama mkombozi wa kulivusha  taifa kuelekea katika haki na usawa kwa watanzania wote.
 
Akiwa njiani kutokea mkoani  mwanza kuelekea mkoani Geita katika eneo la chato alikozaliwa msafara wa dr magufuli ulijikuta ukisimamishwa njiani mara kwa mara na umati mkubwa wa wananchi bila ya kujali jinsia na rika waliojitokeza barabarani kwa lengo la kutaka kumuona huku wakiwa na matawi ya miti.
 
Akitambulishwa na umati mkubwa wa wananchi katika ofisi za mkoa wa chama hicho mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Joseph Msukuma Kasheku alisema chama hicho hakika hakikukosea kumteua Dr. Magufuli kugombea nafasi ya urais kupitia chama hicho kwa kuwa ni kipenzi cha watanzania wote bila ya kujali itikadi za kivyama.

Akizungumza wakati akiwashukuru,kuwaaga na kujitambulisha kwa wananchi waliokusanyika katika ofisi za chama cha mapinduzi mkoani Geita na hatimae vunja jungu katika jimbo la chato, mgombea urais wa CCM Dr.John Pombe Magufuli alikishukuru chama hicho kwa kumuamini na kuongeza kuwa makundi ya wagombea wa nafasi ya urais ndani ya chama hicho yamezikwa rasmi na limebaki kundi moja la umoja ni ushindi.

Wakizungumzia uteuzi wa Dr.Magufuli kugombea kiti hicho cha urais kupitia chama cha mapinduzi baadhi ya wananchi walisema tanzania imepata kiongozi atakayesaidia kuipeleka tanzania katika nchi ya ahadi.
Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia maelfu ya Wanaccm na Wananchi wa Mkoa wa Geita.
Msafara wa Mgombea Urais alieteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye Ofisi za CCM Mkoa wa Geita

0 comments:

Post a Comment

SHARE