Pages

Ads 468x60px

Wednesday, June 7, 2017

Chama cha ACT Wazalendo kimempongeza Rais Dkt. John Magufuli


Chama cha ACT Wazalendo kimempongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa kumteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Anna Mghwira kuwa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na kumshauri asichoke kuteua wengine wanaofaa kutumikia na kujenga taifa.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM, Kaimu Kiongozi wa chama hicho Samson Mwigamba amesema chama hicho kinamtakia kila la heri Anna Mghwira.
Kwa mujibu wa Katiba ya ACT, Anna Mghwira ataendelea kuwa mwanachama japokuwa nafasi yake ya uenyekiti imechukuliwa na Yeremia Kulwa Maganja.

0 comments:

Post a Comment

SHARE