Fundi
 mbao, Japhet Lendiman (38) mkazi wa Daraja Mbili, anashikiliwa na Jeshi
 la Polisi, baada ya kubaka watoto wake wa kike wa darasa la sita na 
kidato cha kwanza.
Akizungumzia
 tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema 
kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kiini cha tatizo hilo 
ni nini na kufuatiwa na hatua ya kufikishwa mahakamani. Mtuhumiwa huyo 
anashikiliwa na Jeshi la polisi tangu Juni 6, mwaka huu na upelelezi 
unaendelea kubaini undani wa tukio hilo.
Akimzungumzia
 mtuhumiwa huyo, mmoja wa majirani wa eneo hilo la Daraja Mbili (jina 
limehifadhiwa) alidai kuwa mzazi huyo amezoeleka kwa tabia hiyo mbaya 
mtaani kwao.
 Alidai
 kuwa mtuhumiwa huyo amezoea kubaka watoto wake mara kwa mara wakati 
mama yao akiwa kazini na kwamba Mei 28 majira ya saa 9:00 alasiri 
alimbaka tena mtoto wake (Jina tumelihifadhi) wa darasa la sita shule ya
 Msingi Daraja Mbili ndipo taarifa zilipoanza kuzagaa mtaani.
“Siku
 hiyo ya tukio lililosababisha mzazi huyo kukamatwa mtoto aliona sasa 
uvumilivu umefika mwisho, alikwenda kwa mama mkubwa na kutoa taarifa 
jinsi baba yake anavyomwingilia na kueleza kuwa anataka kunywa sumu ili 
afe,” alieleza jirani huyo. 
Alisema
 baada ya maelezo hayo mama mkubwa aliamua kuhoji watoto wote wa shemeji
 yake akiwemo mwingine wa umri wa miaka 14 (jina limeifadhiwa) ambaye 
yupo kidato cha Kwanza Sekondari ya Felix Mrema, alikiri kuingiliwa na 
baba yake tangu mwaka 2016. 
Aliendelea
 kueleza kwamba mama yao mkubwa ambaye ni muuguzi (jina limehifadhiwa ) 
katika moja ya hosptali mkoani Arusha, aliamua kutoa taarifa kwa 
mwenyekiti wa mtaa na Polisi.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment