Katibu
Mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo
amewakejeli watu wanaopinga ripoti mbili za mchanga zilizowasilishwa na
tume mbili tofauti za wasomi kwa Rais John Magufuli.
Profesa
Kitila ambaye alikuwa mshauri wa chama cha ACT-Wazalendo, ametumia
mtandao wake wa Twitter kufikisha ujumbe wake kwa watu aliodai wanapinga
kila kitu.
“Kuna
ugonjwa unaitwa opposition defiant disorder (ODD). Dalili kubwa ni
kupinga kwa lengo la kupinga hadi unajipanga mwenyewe. Tuuepuke!,” aliandika Profesa Mkumbo.
Mkumbo
aliandika wazo hilo baada ya kuwepo baadhi ya watu walioonekana kupinga
ripoti na maamuzi ya kamati iliyoongozwa na Profesa, Nehemiah Osoro.
Hata
hivyo, watanzania wengi ikiwa ni pamoja na wasomi wameonesha kuunga
mkono ripoti hiyo na mapendekezo yote yaliwasilishwa, ambayo Rais John
Magufuli aliahidi kuyafanyia kazi yote.
0 comments:
Post a Comment