Pages

Ads 468x60px

Sunday, June 11, 2017

USAJILI SIMBA 11 JUNE 2017, SIMBA KUNASA FUNDI HUYU

Image result for SIMBA SC


KIWANGO cha kiungo wa AFC Leopards, Allan Kateregga kwenye michuano ya Super Cup, kimewavuta Simba na sasa wanataka kunasa saini ya nyota huyo wa Kenya.

Kiungo huyo aliingia kipindi cha pili katika mchezo wao wa Super Cup dhidi ya Singida United na kutoa pasi ya bao kwa Vincent Oburu aliyeisawazishia timu yake na kutinga nusu fainali kwa mikwaju ya matuta 5-4, akiwamo kwenye orodha ya wapigaji.


Katika mchezo wa nusu fainali aliisumbua sana safu ya ulinzi ya Yanga, ingawa mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 0-0 na Leopards kutinga fainali kwa kushinda mikwaju ya penalti 4-2, ambayo pia Kateregga alipiga na kumtesa mlinda mlango Deogratius Munish ‘Dida’.

Pamoja na Simba kunyemelea saini ya mchezaji huyo, nao Singida United wanataka kuendelea kujenga kikosi chao kwa kumnasa mchezaji huyo.

Akizungumza na chanzo chetu, Kateregga alisema tayari ameanza kufanya mazungumzo na viongozi wa Simba na Singida United wakitaka asajili kwenye klabu kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Nimefanya mazungumzo na viongozi wa Simba na Singida United, lakini viongozi wa Simba ndio nawaona kama wanahitaji zaidi kunisajili. Kwahiyo nawasubiri tuweze kukubaliana na kucheza Tanzania,” alisema Kateregga.

Kateregga aliongeza kuwa mkataba wake na AFC Leoprad umebakisha miezi sita kumalizika, hivyo kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) zinamruhusu kufanya mazungumzo na klabu yoyote inayohitaji kumsajili.

“Nimebakisha miezi sita kumaliza mkataba wangu, niko huru kufanya mazungumzo na timu yoyote kwa hiyo nasubiri michuano hii iishe ili niweze kumalizana na viongozi wa Simba,” aliongeza Katerega.

Simba wakifanikiwa kunasa saini ya mchezaji huyo watakuwa wamekwishafanya usajili wa wachezaji kadhaa kama John Boco ‘Adebayor’ aliyemaliza mkataba wake Azam FC, Yusuph Mlipili (Toto Africans) na Jamal Mwambeleko (Mbao FC)

0 comments:

Post a Comment

SHARE