Serikali
imetoa takwimu ikielezea hali ya ukuaji uchumi katika kipindi cha mwaka
2016 na kueleza kuwa kiwango hicho kimeendelea kukua kwa wastani wa
asilimia saba ikiwa ni pungufu kidogo ya kile kilichotarajiwa awali.
Akisoma
hotuba ya mwelekeo wa hali ya uchumi wa Taifa bungeni leo Alhamisi,
Waziri wa Fedha na Mpango , Dk Philip Mpango amesema makadirio ya awali
yalionyesha kuwa uchumi huo ungekua kwa wastani wa asilimia 7.2.
“
Hali ya ukuaji uchumi imeendelea kushuhudiwa katika kiwango kilekile
cha awali cha asilimia saba na hii imechangiwa na mambo mengi ikiwamo
baadhi ya sekta kutofanya vizuri,” amesema.
Ametaja
baadhi ya sababu hizo kuwa ni pamoja na kushuka wa sekta ya kilimo
iliyotarajiwa kukua kwa asilimia 2.9, lakini malengo hayo hayakufikiwa
na badala yake yalikuwa kwa asilimia 2.1.
Pia,
amegusia sekta ya biashara aliyosema ilikuwa kwa asilimia 6.7 hali
ambayo ni tofauti na makadirio yaliyowekwa awali yaliyokuwa asilimia
7.8.
Eneo la chakula nalo limetajwa kuchangia kushindwa kufikia kwa malengo ya ukuaji wa uchumi.
“Makadirio yetu yalikuwa kwamba sekta ya chakula ingekua kwa asilimia nane, lakini bahati mbaya ilishuka na kuwa asilimia 3.7,”amesema.
Hata
hivyo, alikumbusha namna sekta nyingine zilivyoweza kufanya vizuri na
kusaidia uchumi wa Taifa kuendelea kuhifadhi kiwango chake. Baadhi ya
sekta hizo ni pamoja na habari na mawasiliano, madini na kiashirio cha
kuendelea kukua kwa sekta ya viwanda.
0 comments:
Post a Comment