Mkazi
 wa Malampaka mkoani Simiyu, Benedictor Bulobo (30) , ametupwa gerezani 
atakakotumikia kifungo kwa miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya 
kumbaka binti wa miaka tisa.
 Alihukumiwa 
 na Mahakama ya Wilaya ya Maswa juzi na Hakimu Mwandamizi Mfawidhi  
Agatha Chigulu, baada ya kuridhishwa  na ushahidi uliotolewa na upande 
wa mashtaka.
Akitoa
 hukumu hiyo hakimu huyo alisema kuwa anatoa adhabu hiyo ili kukomesha 
vitendo hivyo na kuwaonya wenye nia  mbaya ya kutaka kutenda kosa kama 
hilo wajifunze na kuacha mwenendo huo.
Chigulu
 alieleza kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 131 cha sheria ya 
kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
 Awali
 mahakama iliambiwa na  Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Nassibu Swedy 
kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 23 mwaka jana  saa 5:00 
asubuhi.
Alimnajisi
 mtoto huyo  maeneo ya nyumbani kwake baada ya kumkamata  kwa nguvu 
binti huyo mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Msingi 
Malampaka na kumwingiza chumbani kwake alipombaka.
Alisema
 mtoto huyo  alipata maumivu makali  baada ya kuumizwa  sehemu za siri, 
 alipiga kelele kuomba msaada na watu walifika katika eneo la tukio,  
kumkamata  na kumfikisha Bulobo katika kituo cha polisi Malampaka.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment