Zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa
kielektoronik BVR umelalamikiwa na wananchi katika manispaa ya Kigoma
Ujiji kutokana na kuchelewa kuandikishwa licha ya wananchi kulala kwa
zaidi ya siku mbili katika vituo vya kuandikishia.
Zoezi
la uandikishaji wapiga kura kwa kutumia mfumo huo limeanza katika kata
za Kagera, Buhanda, Businde, Machinjioni, Rubuga na Kasimbu huku kata
nyingine zikisubiri awamu ya pili hali ambayo inawafanya wananchi wa
kata nyingine kwenda kujiandikisha katika kata zilizoanza zoezi hilo
kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi.
Kutokana na hali hiyo wameomba kuongezwa kwa muda wa uandikishwaji wapiga kura na kuweka utaratibu mzuri ambao utawezesha wananchi wote wenye sifa kuandikishwa
Kwa upande wake afisa mwandikishaji msaidizi katika kata ya Buhanda Sufiani Baruani amesema zoezi hilo linakabiliwa na tatizo la idadi kubwa ya wananchi kulingana na uwezo wa mashine zilizopo.
Awamu ya kwanza ya uandikishaji wapiga kura mkoani Kigoma imeanza katika baadhi ya kata Mei 21 huku ikiripotiwa kusimama kwa zoezi hilo katika kata ya Nguruka kutokana na kuishiwa kadi huku maelfu ya wananchi wakiwa bado hawajaandikishwa.

0 comments:
Post a Comment